• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ziara ya rais wa China Mashariki ya Kati kulenga mchango wa China katika amani ya kanda hiyo

    (GMT+08:00) 2016-01-19 10:35:06

    Rais Xi Jinping wa China leo anaanza ziara ya siku tano katika nchi tatu za Mashariki ya Kati, itakayomfikisha Saudi Arabia, Misri na Iran. Mbali na mambo ya ushirikiano kati ya pande mbili, ziara yake pia inatarajiwa kuangalia mchango wa China katika kuhimiza amani na maendeleo katika eneo la Mashariki ya Kati. Xie Yi na maelezo zaidi

    Naibu waziri wa mambo ya nje wa China Bw Zhang Ming jana akiongea ziara alisema, rais Xi anatarajiwa kukutana na mfalme wa Saudi Arabia Salman bin Abdulazizi Al Saud na Rais Hassan Rouhani wa Iran, na atatoa hotuba kwenye makao makuu ya Umoja wa Nchi za Kiarabu mjini Cairo. Ziara yake itaweka wazi sera za China na mapendekezo ya kuhimiza amani na maendeleo katika eneo la Mashariki ya Kati.

    Mjini Riyadhi, Rais Xi pia atakutana na katibu mkuu wa Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba Bw Al Zayani na katibu mkuu wa Jumuiya ya nchi za Kiislamu Iyad Ameen Madani. Bw Zhang amesema China inashikilia kufuata msimamo ulio wa haki na wenye uwiano wa kuhimiza amani na utulivu katika eneo la mashariki ya kati, na kupitia ziara hiyo itaendelea kuhimiza mawasiliano kati ya nchi za mashariki ya kati ili kupunguza hali ya wasiwasi katika eneo hilo.

    Nchi tatu anazotembelea Rais Xi, zote ni nchi zenye ushawishi mkubwa katika eneo la mashariki ya kati, Bw Zhang amesema Rais Xi atajadiliana na viongozi wa nchi hizo kuhusu mambo nyeti yanayolikabili eneo hilo ikiwa ni pamoja na mapambano dhidi ya ugaidi. Bw Zhang amesema China na nchi za mashariki ya kati wote ni wahanga wa ugaidi, na ni wadau katika mapambano dhidi ya ugaidi. Kwa hiyo watajadiliana mambo kuhusu ushirikiano kwenye eneo hilo.

    Ziara ya Rais Xi inafanyika wakati China imetoa waraka kuhusu uhusiano kati yake na nchi za kiarabu, unaosisitiza uhusiano wa jadi kati ya pande mbili, na kueleza kuwa uhusiano huo utaimarishwa. Hii ni hatua nyingine ya kuhimiza uhusiano kati ya China na nchi za kiarabu baada ya baraza la ushirikiano kati ya China na nchi za kiarabu lianzishwe mwaka 2004.

    Ziara ya Rais Xi pia inafanyika wakati mkutano kati ya vyombo vya habari vya China na vya nchi za kiarabu unafanyika mjini Cairo, ukiwa na lengo la kuhimiza ushirikiano kati ya pande hizo mbili

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako