• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Mashariki ya Kati zinakabiliwa na fursa za kihistoria katika ushirikiano

    (GMT+08:00) 2016-01-19 16:59:45

    China na Mashariki ya Kati zinakabiliwa na fursa mpya za kihistoria katika ushirikiano kati ya pande hizo mbili, wakati rais Xi Jinping wa China anaanza ziara kwenye nchi za Saudi Arabia, Misri, na Iran.

    Hayo yamo kwenye makala iliyochapishwa leo kwenye gazeti la People's Daily la China. Gazeti hilo limesema, kuaminiana kisiasa na ushirikiano wa kimkakati kati ya China na Mashariki ya Kati vinaongezeka kidhahiri.

    Katika miaka mitatu iliyopita, rais Xi, katika matukio ya pande mbili na pande nyingi, alitilia mkazo uhusiano kati ya China na nchi za Mashariki ya Kati. Pande hizo pia zinaungana mkono katika kuhimiza pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja, kuinua ushirikiano katika ujenzi wa miundo mbinu, na kuanzisha ukuaji mpya wa uchumi na ajira ili uchumi wa pande hizo uweze kukabiliana na hatari.

    Makala hiyo imesema, China inapinga kithabiti jaribio lolote la kuunganisha vitendo vya kigaidi na dini au nchi fulani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako