• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China na Saudi Arabia kuinua ngazi ya ushirikiano kati yao na kuangalia zaidi ushirikiano kwenye mambo ya viwanda.

    (GMT+08:00) 2016-01-20 09:04:15

    China na Saudi Arabia zimekubaliana kuinua ngazi ya ushirikiano kati yao na kuwa ushirikiano wa kina wa kimkakati na kuangalia zaidi ushirikiano kwenye mambo ya viwanda.

    Pande mbili zimesaini makubaliano kwenye ushirikiano wa mambo ya viwanda, baada ya mazungumzo kati ya Rais Xi Jinping na Mfalme Salman Abdulaziz. Kwenye makubaliano hayo pande mbili zimekubaliana kushirikiana kwenye mkakati uliopendekezwa na China wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja"

    Rais Xi pia amekutana na katibu mkuu wa Umoja wa Nchi za Kiislamu OIC Bw Iyad Ameen Madani na kusema OIC ni alama ya umoja kati ya nchi za kiislamu na umetoa mchango mkubwa kwenye ushirikiano kati ya nchi hizo. Amesema katika muda wa zaidi ya miaka 40 China na OIC zimewasiliana vizuri, na kupata njia ya tamaduni tofauti, dini tofauti na mifumo tofauti kuelewana.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako