• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China akutana na katibu mkuu wa jumuiya ya ushirikiano wa kiislam

    (GMT+08:00) 2016-01-20 21:27:27

    Rais Xi Jinping wa China amekutana na katibu mkuu wa jumuiya ya ushirikiano ya kiislam Bw. Iyad Ameen Madani mjini Riyadh.

    Rais amesema China na nchi za kiislam zina uhusiano mzuri na urafiki wa jadi. Rais Xi Jinping amesisitiza kuwa, China inapenda kuimarisha ushirikiano na nchi za kiislam, kulinda kwa pamoja maslahi halali ya nchi zinazoendelea, kusukuma mbele mageuzi kwa usimamizi wa dunia na kuhimiza amani na maendeleo duniani.

    Kwa upande wake, Bw. Iyad amesema jumuiya hiyo inazingatia sana uhusiano kati yake na China, na ina msimamo unaofanana na China katika kushughulikia mambo ya kimataifa. Amesema jumuiya hiyoinatarajia kuwa China itafanya kazi muhimu zaidi katika mambo ya Mashariki ya Kati na ya Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako