• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Misri wakutana

    (GMT+08:00) 2016-01-21 09:22:34

     

    Rais Xi Jinping wa China amekutana na Rais Abdel-Fattah al-Sisi wa Misri mjini Cairo na kusema China inapenda kushirikiana na Misri kuhimiza utaratibu wa kimataifa uwe wa haki na wenye usawa zaidi kwenye msingi wa kusaidiana na kuheshimiana.

    Rais Xi amesema China inaunga mkono juhudi za Misri za kulinda utulivu, kukuza uchumi, kuboresha maisha ya watu na kutoa mchango mkubwa zaidi katika mambo ya kikanda na ya kimataifa. Rais Xi amesisitiza kuwa nchi zinatakiwa kufuata njia zinazoendana na historia, desturi na hali halisi ya maendeleo ya kiuchumi, kwa hiari ya wananchi wa nchi hiyo na kuhimizwa hatua kwa hatua. Ameeleza matumaini yake kuwa China na Misri zitadumisha na kuendeleza vizuri urafiki wa jadi kati yao na kuwawezesha watu wa pande mbili wanufaike na maendeleo ya uhusiano wa pande mbili.

    Kwa upande wake, rais Abdel-Fattah al-Sisi amesema Misri inapongeza mafanikio ya China katika kujiendeleza, na inapenda kuiga uzoefu wa China, kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika sekta mbalimbali na kuhimiza uhusiano wa kina wa wenzi wa kimkakati kati ya Misri na China.

    Kwa nyakati tofauti, rais Xi Jinping wa China jana pia alikutana na waziri mkuu wa Misri Bw. Sharif Ismail.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako