• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China na mfalme wa Saudi Arabia wahudhuria sherehe ya uzinduzi wa kiwanda cha mafuta cha Yasref

    (GMT+08:00) 2016-01-21 09:23:09

    Rais Xi Jinping wa China na mfalme Salman bin Abdulaziz Al Saud wa Saudi Arabia jana mchana walihudhuria sherehe za kuzindua kiwanda cha mafuta cha Yasref, mradi mkubwa zaidi wa uwekezaji wa China nchini Saudi Arabia.

    Rais Xi amesema ushirikiano wa nishati kati ya China na Saudi Arabia umetoa manufaa makubwa kwa wananchi wa nchi hizo mbili, na uzinduzi wa kiwanda hicho unahimiza sio tu mkakati wa maendeleo ya kitaifa ya Saudi Arabia, bali pia mkakati wa China wa kutekeleza ushirikiano na nchi zilizopo kwenye "Ukanda Mmoja na Njia Moja". Ameongeza kuwa nchi hizo mbili zitakuwa na miradi mingi ya pamoja, ambayo itaimarisha ushirikiano wa biashara na nishati na kuhimiza uhusiano wa kina wa wenzi wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili.

    Baada ya sherehe hizo za uzinduzi, rais Xi alikuwa amekamilisha ziara yake ya siku mbili nchini Saudi Arabia na kwenda nchini Misri kuendelea na ziara yake ya nchi tatu za Mashariki ya Kati, ambayo pia itamfikisha Iran.

    Katika ziara yake nchini Saudi Arabia, rais Xi pia alitembelea Kasri la Murabba, lililopewa jina baada ya muundo wa eneo lake la mita 400 kwa 400 lililojengwa na mfalme Abdul Aziz Ibn Saud.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako