• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi aeleza sera ya China kuhusu Mashariki ya Kati

    (GMT+08:00) 2016-01-22 09:53:05

    Rais Xi Jinping wa China jana mjini Cairo alitoa hotuba kwenye makao makuu ya Jumuiya ya Nchi za Kiarabu na kueleza sera ya China kuhusu Mashariki ya Kati. Akiwahutubia viongozi mbalimbali wa mashirika na nchi za Mashariki ya Kati akiwemo katibu mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Bw. Nabil el-Araby jana kwenye makao makuu ya Jumuiya hiyo.

    Kwenye hotuba yake Rais Xi alizungumzia mambo ya siasa, uchumi na usalama, na alisisitiza kuwa China inapenda kuhimiza amani na maendeleo ya ukanda huo.

    "Mashariki ya Kati ni eneo lenye utajiri mkubwa, lakini kinachosikitishwa ni kuwa hadi sasa bado halijaondokana na vita na mapigano. Watu wa kanda hii wanatarajia kuona machafuko na taabu vinapungua na utulivu na heshima vinaongezeka. Mashariki ya Kati ni eneo lenye matarajio, na pande zote zinapaswa kutafuta matarajio hayo katika njia za kutafuta mazungumzo na maendeleo."

    Rais Xi amesema mazungumzo ni njia muhimu ya kuondoa tofauti, maendeleo yanaweza kusaidia kutatua matatizo magumu na chaguo la njia linapaswa kuendana na hali halisi ya taifa.

    "Nchi mbalimbali zinatakiwa kufuata njia zinazoendana na historia, desturi na hali halisi ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii na kwa hiari ya wananchi wa nchi hiyo"

    Rais Xi pia amesisitiza kuwa suala la Palestina ni suala la kimsingi kwa amani ya Mashariki ya Kati, jumuiya ya kimataifa inapaswa kuchangia kurudisha upya mazungumzo na kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa, na pia inapaswa kutetea haki na usawa.

    "Ili kuboresha maisha ya Wapalestina, China imeamua kutoa msaada wa dola za kimarekani milioni 7.6 kwa Palestina, na pia kutoa uungaji mkono kwa mradi wa ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya jua cha nchi hiyo."

    Rais Xi pia ameeleza hatua kabambe za sera ya China kuhusu Mashariki ya Kati zilizotolewa kwa kuzingatia maslahi ya watu wa ukanda huo na kutoa wito kwa pande hizo kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja na Njia Moja" katika kipindi muhimu cha miaka mitano ijayo. Amesema China na nchi za kiarabu zinapaswa kujenga ushirikiano wa kimkakati kuhusu nishati kwenye msingi wa kunufaishana, kuvumbua utaratibu wa biashara na uwekezaji, kuimarisha ushirikiano kwenye mambo ya kisasa na kuinua ngazi ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili.

    Rais Xi Jinping wa China jana pia kwa nyakati tofauti alikutana na katibu mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu Nabil el-Araby na rais Abdel-Fattah al-Sisi wa Misri. Kwenye mazungumzo yake na Bw. el-Araby, rais Xi alisema China siku zote inaunga mkono shughuli halali za nchi za kiarabu na juhudi za kuimarisha umoja na kutatua matatizo yao ya kikanda. Bw. el-Araby amesema nchi za kiarabu zinatilia maanani sera ya China kuhusu Mashariki ya Kati na kupenda kuongeza ushirikiano na China katika masuala mbalimbali, ili kuhimiza maslahi ya pamoja ya pande hizo mbili.

    Kwenye mazungumzo na rais al-Sisi wa Misri, rais Xi alisema lengo la ziara yake nchini Misri ni kupanga zaidi maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo, kuimarisha ushirikiano katika maeneo mbalimbali na kuinua ngazi ya ushirikiano kati ya China na Misri. Naye rais al-Sisi alisema Misri inapenda kuunganisha mpango wake wa maendeleo ya kitaifa na mpango wa China wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja", kuhimiza ushirikiano katika miundombinu chini ya utaratibu wa Benki ya Uwekezaji wa Miundombinu ya Asia na kukaribisha makampuni ya China kuwekeza zaidi nchini Misri. Baada ya mazungumzo yao, marais hao wawili walizindua kwa pamoja sehemu ya pili ya eneo la ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara la Seuz kati ya China na Misri.

    Habari pia zinasema kampuni ya ujenzi ya China jana ilipata zabuni ya kandarasi ya ujenzi wa mradi uliopo katika mji mpya wa Misri, wenye thamani ya dola bilioni 2.7 za marekani, ambao ni mradi mwingine muhimu kwa China katika kuhimiza ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako