• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watoto wasaidia kulinda Milu

    (GMT+08:00) 2016-03-01 07:57:37

    Hifadhi ya kitaifa ya Tian'ezhou Milu katika mkoa wa Hubei ilijengwa mwaka 1991 ili kumlinda mnyama aitwaye Milu, ambaye pia anajulikana kama Kulungu Père wa Daudi. Kwa sababu sehemu kubwa ya hifadhi hiyo iko kwenye eneo la mashamba, ni muhimu kwa wenyeji wa eneo hilo kuongeza uelewa wa jinsi ya kumtunza myama huyo.

    Katika miaka ya karibuni, Hifadhi hiyo imekuwa ikishirikiana na shule za eneo hilo kwa kutoa elimu kwa wanafunzi kumlinda mnyama huyo na mazingira.

    Kwa wanafunzi katika Shule hii ya Msingi ya Tian'ezhou, kuimba wimbo wa "Milu, Anakuja Nyumbani" ni njia ya kuanza siku yao kwa furaha. Wimbo huu ulitokana na ndama wa Milu aitwaye Jiaojiao.

    Cai Jiaqi, mkuu wa Idara ya Uenezi wa Elimu iliyo chini ya Hifadhi ya Kitaifa ya Tian'e zhou Milu anasema.

    "Tulipata ndama wa Milu aliyetelekezwa na kusombwa na mafuriko. Tukampa jina Jiaojiao kwa sababu alipatikana katika sehemu inayoitwa Jiao Zi Yuan. Tukamlea na kumrudisha porini alipofikisha miaka miwili na nusu. Kulingana na hadithi hiyo, kituo cha TV cha Hubei kilitengeneza filamu iitwayo 'Milu, Coming Home' na wimbo wa maudhui pia ulikuwa na jina hilo hilo"

    Kuwafundisha wanafunzi wimbo huo sio tu sehemu ya pekee ya jitihada za elimu. Shule pia imefungua darasa ambalo linalenga kutoa elimu kuhusu Milu na jinsi ya kuwalinda. Liu Zhifa, mkuu wa Shule ya Msingi ya Tian'ezhou anaelezea umuhimu wa darasa la aina hiyo.

    "Tunataka kuongeza uelewa wa wanafunzi wa jinsi ya kuwalinda wanyama hao na pia mazingira. Baada ya kuanzisha darasa, visa vya kukamata na kuua wanyama pori vimepungua katika kanda hii.. Hii ni kwa sababu uelewa wa wazazi pia umeongezeka. Wakati Milu wanapoingia katika mashamba yao na kuharibu mazao, badala ya kuwaumiza, wazazi wanajua wanapaswa kuwasiliana na maafisa wa hifadhi kwanza. "

    Bila shaka utoaji elimu umezaa matunda. Pan Ling, mwanafunzi wa daraja kwenye shue hii, anafahamu hasa nini cha kufanya kama Milu ataingia shambani mwao.

    "Kwanza, tunapaswa kumtuliza. Kisha, tunaweza kuwasiliana na wafanyakazi katika hifadhi ili kumchukua."

    Mwanafunzi mwingine Liu Sheng-rong pia anafahamu jinsi ya kushughulikia tukio kama hilo.

    "Tunapaswa kuwafahamisha watu zaidi juu ya Milu. Tunaweza kuwaambia watu wa familia, marafiki, na majirani zetu tunachojua, na wanaweza kuwaambia watu wengi zaidi. Kwa njia hii, sisi wote tutaongeza uelewa wa kulinda Milu. Tunaweza pia kuweka vifaa vya uchunguzi katika mazingira ya Milu. Kama mtu anataka kuwadhuru, wafanyakazi wa Hifadhi wataweza kujua. "

    Walimu pia wametekeleza jukumu muhimu katika kulinda mnyama huyu aliye hatarini kutoweka.

    Ding Xiangyu kutoka Shule ya Msingi ya Tian'ezhou anasema mara kwa mara anawataka wanafunzi kuzungumzia hisia zao kuhusu Milu na jinsi ya kumlinda mnyama huyo baada ya darasa. Anasema anataka wanafunzi wajue hakuna jitihada ndogo.

    "Chukua shule kama mfano. Kama wanafunzi wakitupa takataka hovyo, nawaambia wasifanye hivyo kwa sababu inachafua mazingira yetu. Na kama baadhi wazazi wanakata miti au kuchoma maua nawaambia wanafunzi wakawashawishi wazazi wao wasifanye hivyo, kwani inaleta uchafuzi wa hewa na uharibifu wa mazingira ya Milu. "

    Pia Hifadhi hii inapanga kuwaelimisha watoto kulinda Milu na mazingira. Li Pengfei ni mtafiti mwandamizi kutoka Reserveonce ambaye wakati mmoja alisoma kwenye taasisi ya Bristol Zoo nchini Uingereza. Anasema jambo muhimu zaidi ya alilojifunza ni kwamba ulinzi wa wanyama unaanza na watoto.

    "Kwenye bustani ya Bristol, walitoa kipaumbele swala la kuongeza uelewa kwa watoto, kulinda wanyama na mazingira. Niliona wanyama huko hawaogopi watu, lakini hapa nchini China mambo ni tofauti. Hakuna kununua, hakuna kuua. Niliporudi kwenye hifadhi hii, nilitaka watoto wetu kujua hilo pia. "

    Li Pengfei anasema Hifadhi hiyo inalenga kuweka utalii wa mazingira katika ajenda yake na mipango ya kukaribisha watoto na kuifahamisha dunia hadithi ya Milu.

    Anaongeza kuwa kila mtu katika kanda hiyo anatakiwa kubeba jukumu la kulinda Milu na mazingira, na hii ndiyo sababu Hifadh ya Tian'ezhou inatoa wito kwa watu zaidi wenye nia kama hiyo kujiunga nao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako