• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mageuzi ya uchumi wa China kutoka 'kiwanda cha dunia' hadi 'soko la dunia'

    (GMT+08:00) 2016-02-02 16:46:42

    Katika miaka 30 iliyopita, China imekuwa na sifa ya kuwa 'Kiwanda cha dunia' kwa kuwa na viwanda vingi vya uzalishaji wa bidhaa zinazotumika katika sehemu mbalimbali duani, hasa kutokana na utekelezaji wa sera ya kufungua mlango kwa nje, gharama ndogo ya nguvu kazi na ya matumizi ya ardhi, na kutimiza ongezeko la kasi la uchumi na biashara. Lakini katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na mabadiliko yaliyotokea katika mazingira ya ndani na ya nje, kwa upande mmoja China ilianza kufanya mageuzi ya kiuchumi, kwa upande mwingine imekuwa soko kubwa la matumizi ya ndani linalovutia uwekezaji mwingi kutoka nje, na kuifanya ibadilike kutoka 'kiwanda cha dunia' hadi 'soko la dunia'.

    Hivi karibuni kampuni maarufu ya vitu vya kuchezea na bidhaa za watoto ya Marekani 'Toys R Us' imefungua duka lake la 100 hapa Beijing. Afisa mtendaji mkuu wa kampuni hiyo Bw. Dave Brandon amesema, katika miaka 10 iliyopita, kampuni hiyo ilifungua maduka 100 katika miji 44 nchini China, na inapanga kuongeza maduka zaidi mwaka huu, kwa kuwa soko la China limechukua nafasi kubwa zaidi katika shughuli za kampuni hiyo.

    "Mwaka huu tunapanga kuongeza maduka nchini China hadi 30 au 40, na hili ni lengo la makadirio tu, si la mwisho, tutaanza kazi hii wakati mwafaka kwenye miji inayofaa. Kwa kampuni yetu ya Toys R Us, ni muhimu sana kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya watoto na wazazi wa China kwa vitu vya kuchezea vya ubora wa juu na burudani za nyumbani."

    Matarajio ya Bw. Brandon yanaweza kuwakilisha maoni ya makampuni ya nje yanayojaribu kupanua soko kwenye sekta ya huduma nchini China. Naibu mkurugenzi wa Taasisi ya utafiti ya Wizara ya biashara ya China Xing Houyuan anaona kuongezeka kwa uwekezaji kutoka nje katika sekta ya huduma nchini China kunaonesha soko la China limeanza kuchukua nafasi kubwa zaidi dunaini.

    "Zamani makampuni ya nje yalizalisha bidhaa tu nchini China na kufuatilia zaidi kuziuza kwenye soko la nje, au tuseme yalitumia fursa ya gharama ndogo ya nguvu kazi nchini China. Lakini sasa China imerekebisha muundo wa uchumi wake, kwa upande mmoja tunaendeleza viwanda vya utengenezaji vya kisasa, na sekta ya huduma, kwa upande mwingine, matumizi ya ndani yamekuwa nguvu kuu ya kusukuma mbele ukuaji wa uchumi wa China, kwa hiyo mitaji ya nje na makampuni makubwa ya kimataifa yamekuja yakifuatilia zaidi wateja wa China, na kutoa huduma kwao."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako