• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kutengeneza filamu ya katuni kwa Familia nchini China

    (GMT+08:00) 2016-02-16 08:36:11

    Ikiwa ilitolewa mwishoni mwa Mei, filamu ya katuni kutoka Japan inayoitwa Stand By Me Doraemon iliingiza dola milioni $ 38.3 katika wiki yake ya kwanza, huku watu wazima na watoto wakifurika kwenye majumba ya sinema kuitazama. Doraemon, ambayo ni mfululizo maarufu wa filamu ya katuni inayohusu paka roboti, ni inakumbukwa na watu wengi waliozaliwa mwishoni mwa karne ya 20 na ambao sasa ni wazazi wa watoto wadogo.

    Zhang Yafei, mtangazaji wa kituo cha televisheni cha Shenzhen, ni mmoja wa watu ambao wameingalia Doraemon tagu utotoni.

    "Nilikwenda kutazama Doraemon na imenikumbusha mambo mengi ya utotoni. Nilikwenda na rafiki yangu na wote tulitoka na machozi. Inanifanya nijiulize ni lini sekta ya filamu ya China itatengeneza filamu kama Doraemon."

    Doraemon ni moja tu ya ya filamu nyingi kutoka nje ambazo zimepata mafanikio nchini China. Kati ya filamu za katuni tano zenye faida kubwa nchini China mwaka 2014, moja tu ndio ilitengenezwa na kampuni ya China.

    Katika nafasi ya nne ni Boonie Bears ambayo imeingiza takriban Yuan milioni 247. Nafasi ya juu inachukuliwa na How to Train Your Dragon 2 iliyotayarishwa na kampuni ya Marekani ya Dreamworks. Nyingine tatu pia zilitengenezwa nchini Marekani. Kwa hivyo ni nini kilifanya filamu hizi kuwa maarufu miongoni mwa watazamaji wa China licha ya vikwazo vya lugha na kitamaduni?

    Zhao Rui, Mkurugenzi Mtendaji na Rais wa shirika la Original Force Ltd, ambalo linahusika na uigizaji wa filamu za katuni nchini China, michezo, CGI na teknolojia ya kutengeneza filamu, anatoa maoni yake.

    "Kwenye soko la filamu nchini Marekani, kiwango cha mauzo ya tikeki kwa ajili ya filamu za katuni kiko juu kwa sababu ni burudani kwa familia. Hii ina maana kwamba filamu si tu burudani kwa watoto lakini ni furaha kwa watu wazima pia."

    Tofauti na filamu za Marekani, Zhao Rui anasema filamu za katuni nchini China haziburudishi familia nzima.

    "Hadi sasa, katika soko la filamu nchini China, ubora wa utengenezaji wa filamu za katuni sio wa kiwango cha juu. Ingawa mwanzoni, lengo ni kutengeneza filamu za kufurahisha familia nzima, ni watoto tu wanaweza kuangalia kwa sababu hawawezi kutaka kujua maana ya filamu hiyo. Lakini, watu wazima wanatambua kwamba hiyo filamu si nzuri kwao."

    Hata hivyo, ubora si sababu ya pekee inayopelekea kukosa mafanikio kwenye utengenezaji wa filamu za katuni kwa watu wazima nchini China . Kwa mujibu wa Makamu wa Meneja Mtendaji wa shirika la Kusambaza filamu la Huaxia, Huang Qunfei, masoko pia yana nafasi yake.

    "Siku hizi bado masoko ya filamu za katuni yanalenga watoto. Hivyo njia za jadi za uuzaji zinatumika kama kuweka matangazo kwenye vipindi za watoto hasa wakati wa vipindi vya katuni. Wana matumaini kwamba watoto watashinikiza wazazi wao kuwapeleka kuangalia filamu. "

    Licha ya kuvutia wazazi kuangalia filamu za katuni kupitia watoto wao, kuna njia nyingine ya kufanya aina hii ya filamu iwavutie zaidi wale wanaodhani wamekuwa wakubwa na hawahitaji tena kutazama. Zou Zhengyu, meneja mkuu wa Tencent AC, anasema ili kuvutia mapenzi ya watu wazima, lazima filamu za katuni ziwe na maudhui yaliokomaa.

    "Ni lazima tuondoe dhana kwamba filamu za katuni ni burudani ya watoto tu na hivyo wakati watu wazima wakiziona, hawatakuwa na dhana ya moja kwa moja kuwa ni za watoto. Wakati huo huo, tunaweza kuanza kubuni filamu za katuni zenye mvuto kwa vijana na watu wazima.Wakati tutaanza kuzalisha zaidi na zaidi filamu za katuni ambazo zinafaa kwa vijana na watu wazima tutaweza kuvutia watazamaji tofauti. "

    Lakini kwa mujibu wa Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Original Force, Zhao Rui, suala muhimu zaidi la kuleta mafanikio kwenye filamu ya familia ni hadithi nzuri.

    "Hadithi ni muhimu kwa sababu filamu zinaelezea hadithi. Nahisi kwamba hivi sasa nchini China, tunakosa watunga hadithi wazuri. Tuna wasanii wengi, lakini wengi wao wanafanya kazi katika vitengo vya kunasa filamu na sekta ya kiufundi ya kutengeneza filamu. Tunaweza kujifunza jinsi ya kuboresha filamu kutoka Hollywood lakini hatuwezi kujifunza kuandika hadithi bora kutoka huko. Ni matumaini yangu kwamba tutakuwa na waongozaji na waandishi wa hadithi bora zaidi katika siku zijazo. Hii inaweza kutatua tatizo la kutokuwa na uwezo wa kuwa hadithi nzuri za filamu za katuni."

    Ingawa mahitaji ya filamu za katuni yanaongezeka, sekta ya filamu nchini China bado inakabiliwa na changamoto nyingi katika kutengeneza filamu za ubora wa juu. Lakini kukiwa na vifaa bora na watunga hadithi wazuri, kuna matumaini kwamba filamu yenye mauzo makubwa itazalishwa katika siku zijazo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako