• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China ina imani ya kuhakikisha uchumi wake unakua kwa kasi inayofaa

    (GMT+08:00) 2016-02-04 19:48:49

    Mkurugenzi wa kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Xu Shaoshi jana amekanusha kauli aliyotoa Bw. George Soros kuwa uchumi wa China unadidimia na umeathiri ongezeko la uchumi wa dunia nzima, akisema kuwa kauli hiyo haina msingi wowote na kwamba China ina uwezo wa kuimarisha mwelekeo mzuri wa ukuaji wa uchumi na pia ina imani ya kuhakikisha uchumi wake unaongezeka kwa kasi inayofaa.

    Mwaka 2015 uchumi wa China uliongezeka kwa asilimia 6.9, ambayo ni kiwango cha chini zaidi katika miongo mwili iliyopita. Hivi karibuni mwekezaji mashuhuri George Soros alisema kuwa uchumi wa China umeanza kudidimia na kuathiri uchumi wa dunia nzima. Akizungumzia kauli hiyo, mkurugenzi wa kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Xu Shaoshi amesema kauli hiyo haina msingi wowote.

    "Tangu mzozo wa kifedha uanze mwaka 2008, ongezeko la uchumi limepungua, katika muda mrefu uliopita, kulikuwa na maoni yanayosema kwamba uchumi wa China umedidimia. Naona, China ina raslimali nyingi, mahitaji makubwa sokoni, eneo kubwa la ardhi, na kuinuka kwa ubora wa vifaa vya uzalishaji, mambo hayo yote yanaweza kujibu swali hili. Muhimu zaidi ni kwamba, hali halisi ya uendeshaji wa uchumi wa China katika miaka ya karibuni na katika siku zijazo itathibitisha kwamba maoni hayo si sahihi."

    Bw. Xu Shaoshi amesema, ingawa ongezeko la uchumi wa China limebadilika, lakini bado liko kwenye kiwango mwafaka. Anaona kwamba ongezeko la asilimia 6.9 si mbaya.

    "Kwanza, asilimia 6.9 inalingana na makadirio. Pili, ongezeko la asilimia 6.9 lilitimizwa katika hali ambayo mabadikio makubwa yametokea kwenye uchumi wa dunia, na uchumi na biashara ya kimataifa vimeongezeka taratibu. Uchumi wa Marekani ulifanya vizuri mwaka jana, lakini katika robo ya nne, ukuaji wake pia ulikuwa ni asilimia 0.7 tu, kwa mwaka mzima ulikuwa ni asilimia 2.4. Ukuaji wa uchumi wa Ulaya na eneo zima linalotumia euro ulikuwa asilimia 1 hivi, na Japan pia ilikuwa chini ya asilimia 1. Makundi mapya ya kiuchumi yameanza kuibuka na kukua, katika hali hiyo uchumi wa China pia umeathiriwa. Tatu, ongezeko la asilimia 6.9 lilifikiwa katika hali ambayo China inaharakisha mageuzi ya uchumi. Iwapo tu nafasi za ajira zinatosha na bei ya bidhaa inatulia, China haitafuti ongezeko la kasi la uchumi, naona asilimia 6.9 si matokeo mabaya."

    Akizungumzia kauli kuhusu uchumi wa China kuathiri ongezeko la uchumi wa dunia, Bw. Xu Shaoshi amesema, mwaka jana pato la taifa GDP ya China lilichukua asilimia 15 ya ile ya dunia nzima, takwimu za shirika la fedha la kimataifa IMF pia zinaonesha kuwa uchumi wa China ulichangia asilimia 25 ya ongezeko la uchumi wa dunia, ikiwa imeizidi Marekani. Uwekezaji wa moja kwa moja wa China kwa nje ulifikia dola za kimarekani bilioni 127.6, ambayo ni ongezeko la asilimia 10 kuliko mwaka 2014. Kwa hivyo, China bado ni nguvu kuu ya msukumo kwa ukuaji wa uchumi wa dunia nzima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako