• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yahimiza uvumbuzi wa kisayansi uhudumie mageuzi ya kiuchumi

    (GMT+08:00) 2016-02-05 17:37:13

    Viongozi wa idara za serikali ya China leo wamesema, China inajitahidi kuhimiza uvumbuzi wa sayansi na teknolojia uhudumie marekebisho yanayofanywa kwenye muundo wa uchumi wa China.

    Tangu mwaka jana, kuhimiza uanzishwaji biashara na uvumbuzi kumekuwa mwelekeo unaofuatiliwa kwenye jamii ya China. Takwimu zinaonesha kuwa hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana, China imekuwa na vituo zaidi ya 2500 vinavyotoa misaada kwa kuanzishwa kwa kampuni mbalimbali za sayansi na teknolojia, na vituo zaidi ya 4000 vinavyohudumia kampuni ndogo zinazofanya uvumbuzi. Hata hivyo, naibu inspekta wa idara ya teknolojia ya juu katika kamati ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Shen Zulin anaona, hatua za kuhimiza uanzishwaji biashara na uvumbuzi bado zinakumbwa na matatizo mbalimbali yakiwemo ugumu wa kutekeleza sera husika na uwezo dhaifu wa kufanya uvumbuzi.

    "Kwa sasa bado kuna matatizo mbalimbali, hasa kuna ugumu wa kutekeleza baadhi ya sera husika, pia kuna watu wengi wanaojaribu kuanzisha shughuli zao ambao hawafahamu sera za taifa, bado kuna vizuizi mbalimbali katika kuanzisha biashara na kufanya uvumbuzi, kwa upande huu bado zinahitajika juhudi zetu za pamoja. Kwa hatua ijayo, tutashirikiana na idara husika katika kuboresha mazingira, kujumuisha uzoefu bora wa mafanikio katika sehemu mbalimbali, ili kuharakisha ujenzi wa majukwaa ya kuhimiza uanzishaji biashara na uvumbuzi na kukusanya watu wenye vipaji vya kufanya uvumbuzi."

    Naye naibu waziri wa sayansi na teknolojia wa China Bw. Yin Hejun amesema, hatua ijayo China itahimiza uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia uhudumie kwa ufanisi zaidi mageuzi ya kiuchumi yanayoendelea.

    "Uvumbuzi wa sayansi na teknolojia unatakiwa kufanya kazi ya uongozi, China itaendelea kuhimiza uvumbuzi na kuanzishwa kwa kampuni za sayansi na teknolojia, kugeuza uvumbuzi wa kisayansi uwe bidhaa au huduma halisi, na kuwafanya watafiti wa sayansi na teknolojia wawe nguvu muhimu katika kufanya uvumbuzi na kuanzisha biashara; Wakati huohuo, hatua hizo zinapaswa kuunganishwa kwa karibu na mkakati wa Made in China 2025, na kuhimiza kampuni kubwa zifanye mageuzi na uvumbuzi katika utafiti, uzalishaji, uuzaji, utoaji huduma na usimamizi. Aidha, China pia inapaswa kuhimiza ukuaji wa kampuni ndogo zinazofanya vizuri na kuhimiza uanzishwaji wa sekta mpya."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako