• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi za Afrika zaendelea kufanya sekta ya usafiri wa ndege iwe huria

    (GMT+08:00) 2016-02-12 20:01:53
    Nchi za Afrika zinaendelea na hatua za kufanya sekta ya usafiri wa ndege iwe huria hadi kufikia mwaka 2017.

    Katibu mkuu wa chama cha mashirika ya ndege cha Afrika Bw Elijah Chingosho amesema mjini Nairobi kuwa nchi zinazomiliki asilimia 85 ya huduma za ndege barani Afrika, zimekubali kufungua soko kwa wenzao barani Afrika. Hatua hiyo inaweza kufanya Afrika iwe na soko moja la safari za ndege kabla ya mwaka 2017.

    Hata hivyo Bw Chingosho amesema kuwa changamoto kubwa ya kufungua soko la huduma ya ndege barani Afrika inatoka kwenye nchi zisizo na mashirika ya ndege yenye nguvu, yanayozisukuma serikali za nchi zao kutoruhusu kufungua soko la huduma ya usafiri wa ndege.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako