• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya China yataka watoto walioachwa vijijini walindwe zaidi

    (GMT+08:00) 2016-02-15 20:45:21

    Baraza la mawaziri la China linalojulikana kama baraza la serikali limetoa waraka likitaka watoto walioachwa vijijini baada ya wazazi wao kwenda kutafuta kazi za vibarua mijini walindwe zaidi.

    Kadiri miji inavyoendelea kupanuka nchini China, watu wengi kutoka vijiji wanakwenda mijini kutafuta vibarua na kuishi, na kuwaacha watoto wao vijijini bila ya uangalizi wa wazazi.

    Wataalamu wanasema watoto hao wanatakiwa kulengwa zaidi katika miradi mbalimbali ya serikali kuhusu ulinzi wa watoto na kuzuia uhalifu unaofanywa na watu chini ya miaka 18.

    Waraka huo umeweka bayana kuwa kulinda haki halali za watoto ni wajibu wa serikali za ngazi mbalimbali, na pia ni wajibu wa pamoja wa familia na jamii nzima, na kupendekeza wazazi waende mijini na watoto wao, au angalau mzazi mmoja abaki.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako