• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sera bora zaidi zinatakiwa nchini China kuunga mkono wafanyakazi wanawake wanaosomea sayansi

    (GMT+08:00) 2016-02-23 07:36:31

    Ukosefu wa usawa kwenye nyanja za sayansi, teknolojia, uhandisi, na hesabu unafuatiliwa sana nchini China katika miaka ya karibuni. Sasa kundi la wanasayansi wanawake na wahandisi wanazitaka mamlaka kutoa sera rafiki zaidi ili kuunga mkono wanawake wafanyakazi na wanafunzi wa kike wanaosomea sayansi.

    Ukosefu wa usawa kwenye nyanja za sayansi, teknolojia, uhandisi, na hesabu unafuatiliwa sana nchini China katika miaka ya karibuni. Sasa kundi la wanasayansi wanawake na wahandisi wanazitaka mamlaka kutoa sera rafiki zaidi ili kuunga mkono wanawake wafanyakazi na wanafunzi wa kike wanaosomea sayansi.

    Kuwawezesha wanawake katika ulimwengu wa sayansi ni suala la kimataifa. Siku zote limekuwa kwenye ajenda za mamlaka nchini China, vyuo vikuu, na vituo vya utafiti, lakini bado limekuwa vigumu kutimia katika utamudi wa kifamilia.

    Mtaalam wa mgonjwa ya damu Chen Saijuan ni mhadhiri katika chuo cha Uhandishi cha China.

    "Asilimia arobaini ya wahadhiri nchini China ni wanawake, lakini asilimia ni ndogo inapokuja kwenye ngazi za juu kama wanataaluma. Asilimia ya wanawake wanachukua nafasi za uongozi pia ni ya chini sana"

    Ni asilimia 5 tu ya wanataaluma kwenye chuo cha Uhandishi cha China ambapo Chen anafanya kazi ni wanawake, na kati ya karibu wanataaluma 500 wa chuo hicho, ni wanawake 3 tu ndio wana umri wa chini ya miaka 60. Takwimu zilizopatikana hivi karibuni katika mradi wa utafiti wa kitaifa unaoitwa Project 863, chini ya asilimia 7 ya wajumbe wa kitaalam wa kamati ni wanawake. Wakati katika mradi wa msingi wa utafiti nchini China ulioitwa 973, asilimia 2 ya wajumbe wataalam kwenye kamati ni wanawake. Chen anasema sio rahisi kwa wanasayansi wanawake kutimiza malengo yao ya kazi.

    "Wanawake wanabeba majukumu zaidi ya kijamii na kifamilia, hususan wakati wanapojifungua. Hawana uamuzi mwingine bali kutumia muda mchache kwenye utafiti. Pia hawana nafasi kubwa pale wanapoomba miradi au ufadhili. Hii inaleta athari kwenye maendeleo endelevu ya kazi yao ya kisayansi."

    Chen Saijuan alihusika kwenye kuandika waraka uliowasilishwa kwenye chombo cha juu cha ushauri wa kisiasa nchini China mapema mwaka jana. Pendekezo lake linatoa wito wa kusimamisha muda na ruhusa ya uzazi kwa wahadhiri wanawake.

    "Nafikiri hatua za kueleweka zinatakiwa ili kuwasaidia wahadhiri wanawake, kama kuna uwezekano wa kubadili umri wa mwisho wa baadhi ya tuzo za wanasayansi na muda wa kuandika maombi kwa miradi maalum unaweza kuongezwa kutokana na kujifungua"

    Hatua kadhaa zinazofaa zimetolewa katika miaka ya karibuni. Wanasayansi wanawake wanaruhusiwa kuomba kuongezewa umri wa kustaafu kutoka miaka 55 hadi 60. Taasisi ya kitaifa ya sayansi asilia inaelekeza kutoa kipaumbele kwa maombi ya wanasayansi wanawake wenye sifa katika mchakato wa kupitisha miradi. Pia umri wa mwisho wa wanawake wanaoomba kwa ajili wanasayansi wanawake ambao bado ni vijana ni miaka 40 badala ya 35 kwa wanaume.

    Hata hivyo, watu wanaopenda wanasayansi wanawake wawezeshwe kama Xin Yingmei wanasema, hatua hizo bado haziridhishi. Xin ni mhandisi wa IT na pia mwenyekiti wa bodi ya kampuni kubwa ya IT mkoani Jiangsu, mashariki mwa China.

    "Katika baadhi ya nchi za Magharibi, wahadhiri vijana wanawake bado wana uwezo wa kuendelea na utafiti wao wakati wa likizo ya uzazi na matokeo yao yanatambulika. Lakini nchini China, wahadhiri wanawake wanafanya kazi kwenye taasisi za utafiti na vyuo vikuu, na wanakosa fursa nyingi sana katika kipindi hicho. Pia hakuna nafasi kwa wao kuendelea na utafiti baada ya kujifungua. Nafikiri hii ndio tofauti kubwa sana."

    Wang Jing ni mhandisi wa elektroniki na pia mwenyekiti wa bodi ya kampumi kubwa ya elektroniki kusini mwa China. Anasema ni muhimu zaidi kwa wanawake wanaofanya kazi kwenye nyanja za sayansi, teknolojia, uhandisi, na hesabu kufahamu jinsi ya kuweka uwiano kwenye vipaumbele vyao.

    "Mtu anatakiwa kufanya juhudi na kujitoa mhanga katika njia ya kufikia mafanikio. Kuleta uwiano kati ya kazi na maisha ya familia ni jambo la muhimu zaidi kwa wanawake. Kutokana na mtazamo huu, familia hususan ni muhimu zaidi kwa kuwa inaweza kuwasaidia kihalisi kutimiza mafanikio katika kazi badala ya kuwashusha chini."

    Wale wanaotaka wanawake wawezeshwe zaidi kwenye ulimwengu wa sayansi wanaamini kuwa, ingawa sera nyumbufu za kazi zimetekelezwa nchini China ili kuletaa usawa katika sekta hiyo, bado mambo mengi yanatakiwa kufanywa ili kuwawezesha wanawake kubaki kwenye fani ya sayansi na kusaidia kuchochea ubunifu na uzalishaji nchini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako