• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kijiji kizuri cha Zhongliao mkoani Hainan China

    (GMT+08:00) 2016-02-18 09:25:57

    Kama ukienda kisiwani Hainan kusini mwa China, unaweza kusikia kuhusu kijiji kidogo lakini kizuri huko Sanya. Kijiji hicho chenye mandhari nzuri ya kupendeza kinaitwa Zhongliao, mazingira yake ni mazuri na watu wa huko wanafuata sana maadili na wanaishi kwa furaha. Wanakijiji wa kijiji hicho hawakati mti hata kidogo, na wala hawabomoi nyumba, au kujenga kuta ovyoovyo. Si waroho na wala hawafuati mitindo ya kisasa.

    Kijiji hicho kizuri cha kabila la Wali chenye "milima ya kuvutia na maji ya kupendeza", kiko katika sehemu ya kaskazini ya mji wa Sanya, na ni kijiji cha kwanza cha majaribio cha mradi wa kujenga vijiji vizuri ulioanzishwa na mji wa Sanya. Waandishi wetu wa habari walipoingia katika kijiji hicho, waliona hali ya uchangamfu, wanakijiji wote walikuwa na pilikapilika kwa ajili ya kuendeleza kijiji chao. Naibu katibu wa kamati ya chama ya eneo la Jiyang bibi Fu Wan alifahamisha kuwa, baada ya kutafiti na kurekebisha mara kwa mara mipango ya usanifu, mradi huo wa ujenzi wa kijiji cha Zhongliao ulianza rasmi tarehe 13 Oktoba mwaka jana, na unatarajiwa kukamilika mwezi Juni mwaka huu. Bibi Fu Wan anasema,

    "Wakati vijiji vingi mjini kwetu vilipojenga majengo mengi haramu, kijiji cha Zhongliao kilikuwa hakifanyi hivyo. Hakikuharibu mazingira yake, hivyo kina mandhari nzuri. Kutokana na ubora wake wa kijiografia, ustaarabu mzuri na mazingira nzuri, tunapofanya ujenzi wa vijiji, tunazingatia kuhifadhi hali ya viumbe, mito, maji, na mifereji ya wakulima. Tunataka kukifanya kijiji hicho kiwe kijiji na mandhari ya kuvutia kinachozingatia utamaduni wa kilimo na utamaduni wa kabila la Wali."

    Ingawa kijiji cha Zhongliao kiko karibu na mji wa Sanya, lakini hakuna kelele kama mjini. Mchana kijijini kuku na bata wanatembeatembea, huku mbwa wanapumzika chini ya miti ya Banyan, na maua ya yungiyungi yanachanua mabwawani. Kuhifadhi mazingira ya asili, na kuishi kwa mapatano na maumbile kumekuwa kanuni ya wanakijiji wa kijiji cha Zhongliao. Mwanakijiji Bw. Fu Kaifang anasema,

    "nyumba za kila familia ziko mbali, na eneo la nyumba zetu ni kubwa, hivyo tunapanda miti karibu na ua. Mazingira ya kiviumbe ya kijiji chetu ni mazuri, hivyo viongozi wa serikali walipokuja kufanya ukaguzi, waliamua kuingiza kijiji chetu kwenye mradi wa ujenzi wa vijiji bora, kwa hiyo mwamko wa kijiji chetu kuhifadhi hali ya viumbe ni mkubwa, na mazingira ya kiviumbe nzuri namna hii ndiyo inaweza kuwavutia watalii wengi zaidi, hivyo uhifadhi wa mazingira ni muhimu sana."

    Kutokana na ushawishi mkubwa wa wa kitalii wa Sanya, vijiji vingi vidogo vya karibu vilikuwa vinafuata njia isiyo sahihi ya kujiendeleza, kutokana na kuzingatia zaidi fedha, wanavijiji wa vijiji hivyo waliacha kulima, na kuchagua njia nyepesi zaidi ya kujiendeleza, yaani kukodisha ardhi zao na kupata faida kutoka kwa makampuni. Kutokana na kuhimizwa na shughuli za utalii, vijiji hivyo vya karibu vilikuwa vinastawi, lakini kijiji cha Zhongliao bado kinashikilia mtazamo wake, kila mwanakijiji wa kijiji hicho hataki kuharibu maumbile na uwiano wa kiviumbe.

    Bw. Gao Wencai amekuwa katibu mzee wa kijiji cha Zhongliao kwa miaka mingi. Katika miaka kadhaa iliyopita, Bw. Gao alipoona maendeleo ya kasi ya vijiji vingine, pia aliwahi kuyumbayumba, alifikiria kama kuna njia moja inayoweza kukifanya kijiji chake kiendelee kwa haraka. Vilevile kulikuwa na wakuu wa makampuni waliotoa ombi la kuingia kijijini, na kuahidi kumpa Bw. Gao jengo moja kama zawadi, wakati huo, watu 16 wa familia ya katibu Gao walikuwa wanaishi katika nyumba yenye mita za mraba 100 hivi, na zawadi hiyo ilikuwa inavutia.

    Lakini baada ya kuwaza na kuwazua, katibu Gao alitoa uamuzi anaouonea fahari maishani mwake, alikataa! Katibu mzee aliwahi kuona kwenye televisheni na kusoma magazeti kwamba majengo mengi haramu yote yanabomolewa, na njia kama hiyo ya kutafuta utajiri wa haraka mwishowe ingemfikisha pabaya. Hivyo aliamua kukataa ujenzi haramu, kwani anaamini kuwa hakuna njia ya mkato maishani. Bw. Gao anasema,

    "Hatukwenda kinyume na sheria, hasa mwaka juzi, kwa kupitia mafunzo ya Chama cha Kikomunisti cha China, niliwaza na kuwazua, kama nikifanya hivyo, basi ni aibu kwangu kuwa mwanachama kwa miongo kadhaa. Nikikiuka sheria na kufanya makosa, umri wangu wa miaka 50 ndani ya chama ungekuwa bure, ni vitendo vya kusaliti chama."

    Tofauti na vijiji vingine vya mji wa Sanya, kijiji cha Zhongliao kinakataa usimamizi wa makampuni ya nje, bali kilitumia fedha za serikali kukamilisha ujenzi wa mwanzoni, kuboresha miundo mbinu, kutokata mti hata mmoja, na wala kutobomoa nyumba hata moja. Hakiharibu mazingira, bali kinawanufaisha wanakijiji kwa ujenzi huo pamoja na sera mpya ya ufunguaji mlango na mageuzi, huku kikidumisha maisha yao yenye mazingira mazuri. Naibu katibu wa kamati ya chama ya eneo la Jiyang bibi Fu Wan anasema,

    "Mambo yote yanashughulikiwa na wakulima wenyewe, tunawapa uungaji mkono tu, na kuwasaidia kuboresha miundo mbinu, kujenga vizuri mazingira, ili kukifanya kijiji hicho kiwe kijiji kinachofaa kuishi na kutalii. Hatupangi kukijenga kijiji hiki kuwa sehemu ya vivutio, bali kupitia ujenzi wa mradi wa vijiji vizuri, kwenye msingi wa kudumisha maisha yenye mazingira nzuri, tunawanufaisha wanakijiji kwa ujenzi huo. Kutokana na hali yake ya kijiografia, kijiji chetu kiko nyuma kimaendeleo, hivyo licha ya kuwanufaisha wanakijiji wetu kwa sera ya ufunguaji mlango na mageuzi, pia tunataka kuhimiza maendeleo, hatutaki wanakijiji wapate hasara."

    Kutokana na mtazamo wa "kutoharibu mazingira ya asili wala kuwafanya wanakijiji watengwe", mambo yote ya kijiji hayaamuliwi tena na mtu mmoja tu, bali yanaamuliwa na wanakijiji kwa kupiga kura. Mwanakijiji wa kijiji hicho Bw. Fu Kaifang anasema,

    "Kuna wazo langu la kijiji chetu kutekeleza mradi wa vijiji bora, kwanza nitaongoza na kufanya utalii wa 'furaha ya familia za wakulima' au hoteli ya familia za wakulima katika ua wangu, kwa upande mmoja nataka kuwahamasisha wanakijiji wa kijiji chetu wafanye shughuli zao na kupata mapato. Kwa kufanya hivyo, mapato ya kijiji chetu pia yataongezeka, na kiwango cha maisha ya wakulima pia kitainuliwa. Serikali imetenga fedha nyingi, kwa lengo la kuboresha maisha ya wanakijiji na kuwaongezea mapato yao."

    Wakati uchumi wa kijiji unapoendelezwa kwa kasi, namna ya kudumisha moyo wa uchangamfu pia ni suala jipya linalokabili mradi wa ujenzi wa vijiji bora. Baada ya ujenzi huo kukamilika kwa hatua ya mwanzo, kijiji cha Zhongliao kitajenga darasa la utamaduni wa China, ili kuongoza wanakijiji waelekee kuwa na kiwango kipya cha maadili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako