• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maandamano makubwa ya kusherehekea Sikuku ya Mwaka mpya wa jadi wa kichina yaliyofanyika huko Brussles, Ubelgiji

    (GMT+08:00) 2016-02-18 20:17:14

    Maandamano ya kwanza ya kusherehekea Sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina yaliyoandaliwa kwa pamoja na Ubalozi wa China nchini Ubelgiji na serikali ya mji wa Brussles, yalifanyika hivi karibuni mjini Brussles. Kampuni za China na wanafunzi wanaosoma nchini humo, pamoja na wachina wanaoishi nchini Ubelgiji walishiriki kwenye maandamano hayo. Shughuli hizo zimeleta furaha ya mwaka mpya wa jadi wa kichina mjini humo.

    Uwanja mkubwa ulioko katikati ya Brussles umepambwa kwa taa nyekundu za kichina, huku ngoma za jadi zikisikika kila mahali, na bendera kubwa ya China ikipepea juu ya jengo la makao makuu ya serikali ya mji huo. Kwenya maandamano ya kusherehekea sikukuu yaliyokuwa yakipita kwenye uwanja huo, wakazi wengi wa mji huo walipiga picha pamoja na wasanii waliojipamba kama the Monkey King ambaye ni mmoja wa wahusika wakuu katika riwaya maarufu ya kale iitwayo The Pilgrimage to the West, na warembo wanaovalia mavazi ya jadi ya kichina Chi-pao.

    Balozi wa China nchini Ubelgiji Bw. Qu Xing, naibu meya wa Brussles Bi. Karine Lalieux na mjumbe maalumu wa waziri mkuu wa Ubelgiji, ambaye ni waziri wa kilimo wa nchi hiyo Willy Borsus walipeana salamu za mwaka mpya, kuchora macho kwenye sanamu ya Simba wa kichina, na kuivalisha sanamu maalumu ya mtoto Juliaant mavazi ya jadi ya kichina. Shughuli hizo zilizindua maandamano ya Sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina mjini humo, ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya uhusiano kati ya China na Ubelgiji. Balozi Qu Xing anasema,

    "Mandamano ya leo ni makubwa sana, na ni ya kwanza kufanyika kwenye historia ya uhusiano kati ya China na Ubelgiji katika muda wa karne moja iliyopita. Wachina walikuja hapa wakati wa Vita kuu ya kwanza ya dunia, waliwasaidia watu wa Ubelgiji kupambana na uvamizi wa nchi za nje na kulinda uhuru wao, na wachina wengi walipoteza maisha yao. Baadhi yao walibaki na kuishi nchini humu. Lakini kwenye sehemu ya katikati ya Brussles, kiini cha siasa nchini Ubelgiji, kwenye uwanja mkubwa ulio katikati ya mji huu na katika ukumbi wa halmashauri ya mji huu, ni mara ya kwanza kufanyika kwa shughuli za kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina."

    Kwenye hafla ya uzinduzi wa shughuli hizo, mjumbe maalumu wa waziri mkuu wa Ubelgiji, waziri wa kilimo wa nchi hiyo Willy Borsus amesema, anafurahi kuweza kuhudhuria halfa hiyo muhimu kwa niaba ya serikali ya Ubelgiji.

    "Tunatilia maanani sana shughuli hizi, kwa kuwa tunatilia maanani marafiki zetu wa China walioko nchini Ubelgiji, na ushirikiano kati ya China na Ubelgiji. Urafiki kati ya nchi zetu mbili sio wa maneno tu, bali unaonekana kwa vitendo halisi, na unaonekana kwenye mawasiliano ya mara kwa mara kati ya viongozi wa nchi zetu."

    Wasanii karibu 1000 kutoka China na Ubelgiji walishiriki kwenye maandamano hayo ya kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina, na walionesha ngoma za jadi za kichina, mavazi ya kichina, kungfu, na mambo mengine mengi ya kiutamaduni ya kichina.

    Bw. Terlinde na mke wake ni watalii kutoka Ujerumani walioshuhudia maandamano hayo. Amesema,

    "Maonesho ni mazuri sana, nimewaona wakipita hapa, wakisherehekea mwaka mpya wa jadi wa kichina. Naona yanavutia sana, na yameonesha moyo wa kufanya kazi kwa pamoja."

    Aliyekuwa kiongozi wa shirikisho la wachina wanaoishi nchini Ubelgiji mzee Xia Tingyuan ameishi nchini humo zaidi ya miaka 50. Amesema anaona fahari ya kuweza kutazama maonesho makubwa namna hiyo ya utamaduni wa kichina nchini Ubelgiji.

    "Nguvu ya China inaongezeka siku hadi siku, nchi nyingi pia zimebadilisha mtizamo wao wa kuionea China. Kwa hiyo kufanya shughuli kama hizo, sisi wachina tunaoishi hapa pia tunajivunia, na tunafurahi sana. Wageni pia wanaweza kutazama wachina wakicheza Kungfu na Taiji, hayo ndiyo maendeleo ya kiutamaduni. Hata hawajawahi kwenda China, pia wanaweza kuviona hapa, hili ni jambo zuri."

    Bw. Hong Jianjiang ni naibu mkurugenzi wa Shirikisho kuu la vijana wa China wanaoishi Ulaya, anasema anatumai kwamba shughuli nyingi zaidi za kuonesha utamaduni wa jadi wa kichina zitafanyika katika siku zijazo.

    "Ni mara yangu ya kwanza kushuhudia shughuli kubwa namna hii ya kuonesha utamaduni wa kichina, kweli naona fahari kubwa. Sisi wachina tunaoishi hapa pia tumefanya juhudi nyingi kufanikisha shughuli hizi. Chini ya uongozi wa Ubalozi, shughuli hizi zimeandaliwa vizuri sana, kweli tunafarahi sana. Katika siku za baadaye, natumai shughuli nyingi zaidi za jadi za kichina zitaweza kufanyika hapa, ambapo ni katikati ya Ulaya, ili kuwafahamisha zaidi watu wa hapa kuhusu utamaduni wa China, na kueneza zaidi utamaduni wetu hapa."

    Balozi Qu Xing amesema, mwaka huu ni wa 45 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya China na Ubelgiji, na shughuli nyingi zaidi kama hizo za mawasiliano ya kiutamaduni, zitafanyika katika siku zijazo.

    "Tumeona kwamba wenyeji wengi wa Ubelgiji wameshiriki kwenye shughuli hizi, angalia watoto wa Ubelgiji wakishika bendera ya taifa la China. Kwenye maandamano yetu, pia tumeona mamia ya watu wa Ubelgiji wakicheza kongfu ya kichina wakivalia nguo nyekundu, kweli nimehisi ushawishi mkubwa wa utamaduni wa China, pia wenyeji wengi wamesifu nafasi ya China kwenye jukwaa la kimataifa, wamepongeza maendeleo ya China, na kusifu utamaduni wa China pamoja na historia ya China."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako