• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuongeza nguvu ya kudhibiti uchafuzi wa hewa

    (GMT+08:00) 2016-02-19 18:16:04

    Katika miaka miwili iliyopita, uchafuzi wa hewa umekuwa tishio kwa afya ya wakazi wa sehemu nyingi nchini China, ingawa idara za kuhifadhi mazingira zimetekeleza hatua mbalimbali za usimamizi na kupata maendeleo kiasi, kutatua kabisa tatizo la uchafuzi wa hewa kunahitaji juhudi kubwa za pamoja kwenye jamii. Waziri wa uhifadhi wa mazingira wa China Bw. Chen Jining amesema, mwaka huu China itachukua hatua madhubuti zaidi za kudhibiti uchafuzi wa hewa na kuinua uwezo wa kukabiliana na hali mbaya ya hewa inayosababishwa na uchafuzi.

    Katika miaka ya hivi karibuni, China imetoa sera na hatua mbalimbali za kuzuia na kupunguza uchafuzi wa hewa. Takwimu zinaonesha kuwa, hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2015, utoaji wa hewa chafu yenye sulfur dioxide na Nitrogen oxide kutoka kwenye vituo vya kuzalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe, ulipungua kwa asilimia 47 na asilimia 50. na kiwango cha wastani cha PM 2.5 katika miji 74 iliyotekeleza vigezo vipya vya usafi wa hewa kilipungua kwa asilimia 14.1. Lakini wakati huohuo, tatizo hilo limejitokeza zaidi kwenye baadhi ya sehemu, haswa miji ya Beijing, Tianjin na mkoa wa Hebei. Akizungumzia hali hiyo, waziri wa uhifadhi wa mazingira wa China Bw. Chen Jining amesema, hatua za kuleta joto wakati wa majira ya baridi na uwezo dhaifu wa kukabiliana na hali mbaya ya hewa yenye uchafuzi pia vimeongeza athari ya uchafuzi wa hewa. Hata hivyo, Bw. Chen Jining amesema, tatizo la uchafuzi wa hewa linapaswa kushughulikiwa wakati wa joto ili kuzuia kuwa kubwa wakati wa majira ya baridi, na wizara yake itachukua hatua 6.

    "Kwanza ni kurekebisha mpango wa dharura wa kukabiliana na hali mbaya ya hewa yenye uchafuzi, ikiwemo vigezo vya kuthibitisha ngazi ya tahadhari za uchafuzi haswa katika miji ya Beijing, Tianjin na mkoa wa Hebei, na sehemu mbalimbali zinapaswa kuchukua hatua kulingana na mazingira yao. Pili ni kutoa kipaumbele katika miji inayoathirika zaidi. Tatu ni kuimarisha hatua za usimamizi wa uchafuzi unaosababishwa na viwanda, ikiwemo kutafiti uwezekano wa mpango wa kuvifanya viwanda vifanye uzalishaji kwa nyakati tofauti, na kuvitoza faini ya uchafuzi kwa viwango tofauti kulingana na majira tofauti na hali tofauti. Nne ni kudhibiti matumizi ya makaa ya mawe, ikiwemo kudhibiti ubora wa makaa ya mawe yanayotumiwa; Tano ni kuimarisha udhibiti wa vyanzo vya uchafuzi vinavyoathiri eneo kubwa, ikiwa ni pamoja na mpango wa kupiga marufuku fataki. Sita ni kuongeza uwekezaji, na kuhakikisha fedha zinazohitajika kutekeleza hatua hizo zinapatikana."

    Tarehe 1 Januari mwaka jana, sheria mpya ya kuhifadhi mazingira ilianza kutekelezwa, na tarehe 1 Januari mwaka huu, sheria mpya ya kudhibiti uchafuzi wa hewa ilianza kutumika rasmi. Bw. Chen amesema, mwaka huu wizara yake itatekeleza hatua mbili maalumu za usimamizi, ili kuhakikisha utoaji uchafuzi kwenye viwanda mbalimbali unatimia vigezo kwa mujibu wa sheria hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako