Naibu mkuu wa idara ya usimamizi wa tiba ya jadi ya kichina na dawa za mitishamba ya China Bw. Yu Wenmin leo amesema, mpango wa mwaka 2016-2030 kuhusu maendeleo ya tiba ya jadi ya kichina na dawa za mitishamba umejadiliwa kwenye mkutano wa baraza la serikali ya China.
Mpango huo unasema hadi kufikia mwaka 2020, kila mtu atapata huduma ya tiba ya jadi ya kichina, na hadi kufikia mwaka 2030 China itakamilisha mtandao wa huduma za tiba ya jadi ya kichina. Hii ni mara ya kwanza kwa serikali kuweka mpango kuhusu maendeleo ya tiba ya jadi ya kichina na dawa za mitishamba, na unaonyesha kuwa tiba hiyo imewekwa kwenye mkakati wa taifa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |