Waziri wa biashara wa China Bw. Gao Hucheng ameeleza imani yake kuhusu biashara ya nje ya China baada ya thamani ya biashara hiyo kushuka mwaka jana.
Biashara ya nje ya China iliendelea kushuka kwa mwezi wa kwanza mwaka huu. Akizungumzia mwelekeo huo, Gao amesema biashara ya nje ya China inatakiwa kuangaliwa kwa kuzingatia muktadha wa uchumi wa dunia, hivyo mwelekeo wa biashara hiyo unaridhisha. Amesema China imedumisha hadhi yake ya nchi kubwa zaidi duniani ya biashara ya bidhaa halisi na uuzaji wa nje.
"Kwa kuwa kiwango cha kushuka ni kidogo hasa katika upande wa uuzaji wa bidhaa katika nchi za nje. Kilichoshangaza ni kwamaba thamani ya biashara ya nje ya China ilipungua mwaka jana, lakini nafasi yake kama mwenzi wa kibiashara duniani ilisonga mbele, na mgao wake katika biashara ya kimataifa uliongezeka. Kwa mujibu wa takwimu za awali, mgao huo uliongezeka kwa asiliami 1 kutoka asilimia 12.2 hadi 13.2, ongezeko ambalo ni kubwa zaidi katika miaka iliyopita."
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |