• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mpito wa uchumi wa China kunufaisha uchumi wa dunia

    (GMT+08:00) 2016-02-23 08:52:23

    Naibu waziri wa fedha wa Marekani Nathan Sheets amesema, mpito wa uchumi wa China kuwa ukuaji mpya sio tu unaweka uchumi wake katika ukuaji bora na endelevu, lakini pia unanufaisha uchumi wa dunia.

    Sheets amesema, uchumi wa China unategemea zaidi sekta ya huduma na matumizi ya majumbani, sio tu utaleta uwiano ndani ya nchi hiyo, bali pia utakuwa na uwiano kwa nje na hivyo kupunguza utegemezi wa biashara ya nje. Ameongeza kuwa China imepata maendeleo muhimu katika kuleta uwiano wa uchumi wake, ikiwemo kuchangia matumizi zaidi katika ukuaji wa GDP, uwekezaji wa kasi katika sekta ya huduma na manunuzi, na ukuaji wa kasi wa ajira na kuanzisha biashara. Mageuzi haya yataiwezesha China kuimarisha hadhi yake kama kiongozi wa mahitaji ya dunia na kutoa mbinu bora kwa China kutimiza utaratibu wa mpito na kuweka uchumi wake kwenye msingi endelevu kwa ukuaji mzuri wa siku zijazo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako