Waziri wa biashara wa China Bw. Gao Hucheng amesema, matumizi ya ndani nchini China kwa mwaka huu yataendelea kuongezeka kwa kasi.
Amesema mwaka jana matumizi ya ndani yaliongezeka kwa asilimia 10 ikilinganishwa na mwaka uliotangulia, na yalichangia asilimia 66 ya ongezeko la uchumi wa China. Amesema ongezeko hilo limechangiwa na ongezeko la kasi la mapato ya wananchi, kuboreshwa kwa huduma za jamii na utoaji bora wa bidhaa.
Bw. Gao pia amesema, wizara hiyo itaendelea kuhimiza mageuzi ya utoaji wa bidhaa ili kuinua ubora wa bidhaa na huduma.
Huku uchumi wa China ukijitahidi kuondokana na utegemezi wa uwekezaji na biashara ya nje, matumizi ya ndani, sekta ya huduma na ubunifu zimeibuka kama injini tatu mpya za uchumi wa China.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |