• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya biashara ya China kuharakisha kuhimiza majukumu ya maeneo ya majaribio ya biashara huria kutekelezwa kwa pande zote

    (GMT+08:00) 2016-02-24 09:44:13

    Waziri wa biashara wa China Bw. Gao Hucheng amesema, miongoni mwa mipango minne ya maeneo ya majaribio ya biashara huria iliyotolewa na baraza la serikali la China mwezi Aprili mwaka jana, majukumu ya majaribio yanayotekelezwa na idara mbalimbali za baraza la serikali ni 366, na kiwango cha utekelezaji kimefikia asilimia 80. Bw. Gao amesema, wizara yake itaendelea kuratibu idara mbalimbali na serikali za mitaa, ili kuharakisha kuhimiza majukumu mbalimbali kutekelezwa kwa pande zote.

    Kwenye mkutano na waandishi wa habari, Bw. Gao amesema, kwa ujumla ujenzi wa maeneo ya majaribio ya biashara huria unaendelezwa vizuri, na umepata mafanikio katika sekta nyingi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako