• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kijiji cha kabila la Wayao mkoani Guangdong kinavyoendeleza shughuli maalum kuwasaidia wanakijiji kuondokana na umaskini

    (GMT+08:00) 2016-02-25 08:21:21

    Kijiji cha Lianshui cha wilaya inayojiendesha ya kabila la Wayao ya Liannan mjini Qingyuan mkoani Guangdong ni kijiji chenye milima mingi, na eneo dogo la ardhi isiyo na rutuba kwa ajili ya mashamba. Kabla ya mwaka 2008, kijiji hicho kilikuwa ni kijiji cha watu maskini. Lakini mwaka 2009, mkoa wa Guangdong ulianzisha kazi maalum ya kuleta maendeleo na kuondoa umaskini, na kufanya ujenzi na marekebisho ya barabara na kufanya usafi wa kijiji hicho, ambao uliboresha sura na mazingira ya kijiji hicho. Wakati huohuo, mkoa huo ulifanya kazi ya kuwahamisha wanakijiji kutoka milimani hadi kwenye sehemu za chini, na kuwahamasisha waendeleze shughuli za upandaji wa mikuyu, ufugaji wa nondo wa hariri, na utalii wa vijijini, ili kukifanya kijiji hicho kiwe kijiji kipya chenye utamaduni maalum wa kabila la Wayao. Baada ya hapo, maisha ya wanakijiji wa Lianshui yakaanza kubadilika.

    Katibu wa chama cha kikomunisti cha kijiji cha Lianshui Bw. Pan Zehui alifahamisha kuwa, kutokana na uungaji mkono mkubwa wa serikali ya mkoa wa Guangdong, katika miaka ya hivi karibuni, shughuli mbalimbali za kijiji cha Lianshui zimepata maendeleo makubwa. Bw. Pan anasema,

    "Mapato ya jumla ya kijiji chetu kwa mwaka jana yaliongezeka hadi kufikia Yuan laki 2.25 kutoka Yuan chini ya elfu 40 za zamani; mwaka jana mapato ya wanakijiji kwa mwaka pia yaliongezeka hadi Yuan 8,200 kutoka Yuan 2,400 za mwaka 2008. Aidha, kijiji chetu cha Lianshui pia kimeanzisha mradi wa 'kijiji kimoja chenye vitu vinne mashuhuri', yaani kupanda mikuyu na kufuga nondo wa hariri, kupanda camellia, kufuga nguruwe wa Yaolin na utalii wa vijijini."

    Mradi huo wa "kijiji kimoja chenye vitu vinne mashuhuri" ulipoanza kutekelezwa, wanakijiji ambao hawakufahamu undani wa mradi huo walikuwa na mashaka. Kwa hiyo viongozi wa kijiji cha Lianshui waliunda kikundi, na kujaribu kutekeleza mradi huo kwanza, na kupata mafanikio. Bw. Pan Zehui anasema,

    "Wakulima wengi waliogopa hatari, hawakuthubutu kujaribu na kutekeleza mradi huo. Sisi tukiwa viongozi tulijaribu kwanza na kuona njia hii ni sahihi, na inaweza kuhimiza maendeleo ya kilimo na ufugaji, na kuendelezwa kwa pamoja; kama hakuna faida basi tuliacha, wanachama wanaongoza kufanya shughuli za umma."

    Kutokana na kuhamasishwa na viongozi wa kijiji, hivi sasa familia 10 za kijiji cha Lianshui zimeanzisha mradi wa utalii wa vijijini. Mwanakijiji Tang Haosangui ni mmoja wao. Katika mwaka juzi, Bw. Tang Haosangui aliacha kazi ya vibarua aliyoifanya kwa miaka 12, na kurudi kwao. Alianza kufanya shughuli za utalii wa vijijini, kwa kupitia vitoweo maalum vya wakulima, hoteli na uuzaji wa mazao ya kilimo, hivi sasa anaweza kuongeza mapato yake kwa Yuan 8,000 kila mwaka, vilevile amevutia watalii wengi kutoka Guangzhou, Foshan na Hongkong. Bw. Tang Haosangui anasema,

    "Kama karanga, viazi vitamu, maboga na mahindi, hayo yote tunapanda wenyewe, na yananunuliwa sana wakati wa sikukuu. Katika siku za kawaida, gharama ya kukaa katika hoteli yetu ni Yuan 50 kwa siku, na Yuan 120 kila siku wakati wa sikukuu. Chakula kinagharamu Yuan 40 hadi 50 kwa kila mtu, kuna vitoweo nane na bakuli moja la supu, pia wanaweza kuonja mvinyo wa matunda ya mikuyu. Mwezi Mei mwaka jana watalii kadhaa kutoka Hongkong walikuja hapa kwa wiki moja na walivutiwa hata hawakutaka kuondoka."

    Wakati mwandishi wetu wa habari alipofanya mahojiano, alikuta mtalii kutoka mkoa wa Henan Bw. Li aliyekuja kujionea mila na desturi za kabila la Wayao za kijiji cha Lianshui. Bw. Li alifahamisha hisia zake kutalii huko,

    "Nilipata habari kuhusu kijiji hicho kutoka kwenye mtandao wa internet, na kufahamishwa na marafiki zangu. Niliuliza wapi kuna kijiji kizuri cha kale karibu na Guangzhou, wakasema kijiji cha kabila la Wayao ni kizuri. Baada ya kujionea, naona kweli sehemu hii ni maalum."

    Licha ya utalii wa vijijini, shughuli za kupanda mikuyu na kufuga nondo wa hariri pia zinaendelezwa vizuri katika kijiji cha Lianshui. Bw. Tang Yamugui ameshughulikia mambo hayo kwa miaka mitano. Anakodi hekta 0.66 za mashamba kwa ajili ya kufuga nondo wa hariri, na kila mwaka anaweza kupata Yuan elfu 20 hadi 30 za ziada. Anasema,

    "Ninafuga nondo wa hariri kila mwezi Mei hadi Oktoba, kila mwaka ninafuga kwa miezi 6. Majani ya mikuyu yanaanguka wakati wa baridi. Mwaka jana bei ya majani ya mkuyu ilikuwa Yuan 8 kwa kilo, nikiuza majani hayo kwa makampuni ya wilaya, napata Yuan elfu 25. Aidha nikiuza majani hayo kwa familia za wakulima kupikia vitoweo, kila mwezi napata Yuan 1200."

    Utekelezaji wa mradi wa "kijiji kimoja chenye vitu vinne mashuhuri" na ujenzi wa aina mpya ya kijiji cha kabila la Wayao vimeongeza mapato ya wakulima, na pia vimeboresha maisha ya wanakijiji wa kijiji hicho, lakini wakati huohuo kijiji hicho pia kinakabiliwa na changamoto ya kulinda utamaduni wa jadi kwenye mazingira ya maendeleo ya mambo ya kisasa. Kwa upande mmoja, baadhi ya wazee wa kabila la Wayao wameishi maeneo ya milimani kwa muda mrefu, na kuhamia katika aina mpya ya kijiji cha kabila la Wayao huenda kutafanya baadhi ya mila na desturi na utamaduni zao za zamani kutoweza kuendelea; kwa upande mwingine, wimbi la maendeleo ya mambo ya kisasa linaenea kote China, na kijiji cha kale cha kabila la Wayao pia kiko katika mwelekeo wa mageuzi. Baadhi ya wanakijiji vijana wa kabila la Wayao wanatumai kuondoka milima na kuanza maisha mapya. Kugongana kwa mambo ya jadi na ya kisasa kumekuwa ni jambo lisiloweza kuepukika.

    Kuhusu suala hilo, profesa wa kituo cha utafiti kuhusu mkakati wa kimataifa cha Chuo cha chama cha kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Bw. Li Yunlong anasema,

    "Kuhamia kutoka sehemu maskini zenye mazingira mbaya ambayo hayafai kwa binadamu kuishi hadi sehemu inayofaa zaidi na kufanya uzalishaji, kwa upande mmoja inaboresha hali ya maisha, kwa upande mwingine imeathiri njia zao za zamani za maisha na tamaduni zao za jadi. Hali hii inapaswa kuangaliwa kutoka pande mbili, kwa upande mmoja, hali hii ni maendeleo, katika mchakato wa kuendeleza mambo ya kisasa, wanakijiji wa kabila la Wayao hawawezi kupata maendeleo zaidi milimani; kwa upande mwingine, utamaduni na jadi zao pia zinapaswa kuhifadhiwa. Uhifadhi huo sio kudumisha hali ya zamani, bali kuendeleza utamaduni mpya wa kabila la Wayao kwenye msingi wa jadi zao."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako