• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China ina uzoefu wa kukabiliana na hatari za kifedha

    (GMT+08:00) 2016-02-25 09:42:29

    Waziri mkuu wa China Bw Li Keqiang amesema serikali ya China ina uzoefu wa kukabiliana na hatari za kifedha na ina sera na njia mbalimbali za kukabiliana na hatari zinazotokea.

    Waziri mkuu Li amesema hayo mjini Beijing alipokutana na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia Bw Jim Yong Kim. Bw Li amepongeza ushirikiano uliopo kati ya China na Benki ya Dunia, na kusema China itaendelea kutekeleza sera za kuhimiza ongezeko la uchumi kwa kushirikiana na jumuiya ya kimataifa na Kundi la G20.

    Bw Kim amesema nchi zote duniani zinatakiwa kuboresha sera za uchumi kwenye mazingira ya uchumi dhaifu, na kusema China imefanikiwa kuwa na ongezeko la kasi la uchumi kwa kutekeleza mageuzi ya muundo wa uchumi wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako