• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mageuzi ya kina yanasaidia kubadili maisha ya watu wa kawaida nchini China

    (GMT+08:00) 2016-02-26 17:17:40
    Takwimu zilizotolewa na wizara ya elimu ya China zinaonyesha kuwa, zaidi ya wanafunzi elfu 69 kutoka familia maskini vijijini wanafurahia sera mpya ya kujisajili vyuo vikuu iliyoanza kutekelezwa mwaka 2014.

    Mageuzi ya mfumo wa elimu ni sehemu moja ya lengo pana la kuboresha maisha ya wachina wa kawaida. Mwaka 2014, kamati inayoongoza mageuzi ya kina ya pande zote, kwa pamoja na idara za serikali ya China, zilitoa zaidi ya hatua 370 za mageuzi, na kumaliza majukumu 80 makuu yaliyopendekezwa na kamati hiyo mwanzoni mwa mwaka huo.

    Mwaka jana, kasi hiyo iliongezeka, na mageuzi yalifanyika kwenye maeneo mengi zaidi ikiwemo mfumo wa sheria, fedha, na kodi, usajili wa familia, mfumo wa mshahara katika makampuni makubwa yanayomilikiwa na serikali, hospitali za umma, jeshi, na hata kandanda. Njia bora zaidi ya kujaribu kama mageuzi hayo yametimiza lengo lake, ni kufuatilia hisia halisi za watu kuhusu matokeo yake.

    Kwa watoto wengi waliozaliwa kwenye familia maskini nchini China, mtihani wa kuingia chuo kikuu unawapa fursa ya kubadili maisha yao: Kuhitimu chuo kikuu, maana yake ni kuwa na fursa nzuri ya kuajiriwa na kuwa na maisha mazuri.

    Wazazi wa Li Shuo, ambao wanaishi kwenye kijiji kimoja kilichoko mkoa wa Jilin, kaskazini mashariki mwa China, hawakupata elimu ya chuo kikuu. Matumaini yao siku zote ni kuwa, kuna siku mtoto wao ataenda chuo kikuu na kuwa mhandisi. Hivyo Li aliposhindwa mtihani wa kujiunga na chuo kikuu mwaka 2014, hatma ya familia nzima, ambayo inaishi kwa kipato cha dola za kimarekani 760 kwa mwaka, ilikuwa mashakani.

    Mwalimu mkuu wa shule aliyosomea Li aliamua kumsaidia, na kupendekeza kuwa anaweza kuomba kujiunga na vyuo kupitia mfumo maalum wa kujiandikisha, ambao umeandaliwa kwa wanafunzi kutoka familia maskini. Kutokana na hilo, Li alipata nafasi ya kujiunga na chuo kikuu cha sayansi na teknolojia cha Changchun, pia alifahamishwa kuwa anaweza kupata ruzuku ya ada ya masomo.

    Katika kijiji kingine cha Hepu kilichoko mkoani Anhui, maisha ya Wang Shousen pamoja na wanakijiji wenzake yamebadilika kutokana na mfumo mpya wa umiliki wa ardhi. Wang, mwenye miaka 50, alikuwa anafanya kazi za vibarua, lakini sasa anakodisha zaidi ya eka 260 za ardhi, na hii inatokana na kanuni mpya zinazowawezesha wakulima kukodisha ardhi yao kwa watu wengine.

    Wanakijiji 1000 waliokodisha ardhi zao kwa Wang, sasa wana nafasi zaidi ya kufanya kazi kwa wengine, na wanafurahia kupata kipato cha ziada.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako