• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idadi wa watu masikini vijijini nchini China imepungua kwa milioni 14

    (GMT+08:00) 2016-02-29 16:35:16

    Takwimu zilizotolewa na Mamlaka ya Takwimu ya China zimeonyesha kuwa, mwaka jana China imefanikiwa kupunguza idadi ya watu masikini vijijini kwa milioni 14.42 na kufikia milioni 55.75.

    Taarifa iliyotolewa na Mamlaka hiyo imeonyesha kuwa, zaidi ya wakazi milioni 17 wa vijijini walipokea posho ya kujikimu kwa mwaka jana.

    Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Xu Xianchun amesema, tofauti kati ya maeneo ya vijijini na mijini imeendelea kupungua kwa mwaka jana. Kipato cha watu wa mijini kilikuwa mara 2.73 zaidi ya wale wa kijijini, ikiwa imepungua kwa asilimia 2 ikilinganishwa na mwaka 2014.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako