• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China ina imani ya kudumisha utulivu wa hali ya ajira mwaka huu

    (GMT+08:00) 2016-02-29 18:39:31

    Waziri wa raslimali watu na uhakikisho wa kijamii wa China Bw. Yin Weimin leo amesema, mwaka huu China inakabiliwa na ugumu mkubwa kwenye suala la ajira, kwa kuwa hatua za kudhibiti sekta ambazo uzalishaji umezidi mahitaji ya sokoni, zitapunguza idadi ya wafanyakazi kwenye sekta hizo. Amesema katika sekta za chuma cha pua na makaa ya mawe tu, wafanyakazi milioni 1.8 watapunguzwa kazi. Pamoja na hayo, Bw. Yin amesisitiza imani yake ya kudumisha utulivu wa hali ya ajira mwaka huu.

    Waziri wa raslimali watu na uhakikisho wa kijamii wa China Bw. Yin Weimin amesema, kuna mambo matatu yanayosababisha ugumu kwenye suala la ajira mwaka huu.

    "Kwanza, hatua za kurekebisha sekta ambazo uzalishaji umezidi kidhahiri mahitaji ya sokoni, zitasababisha baadhi ya wafanyakazi wapoteze ajira; Pili, uchumi wa China unakabiliwa na shinikizo kubwa la kupungua, baadhi ya kampuni zinakabiliwa na matatizo makubwa katika uendeshaji na uzalishaji; Tatu, idadi ya wahitimu wa vyuo vikuu ambao ni kundi kuu la watu wanaotafuta ajira, bado inaendelea kuongezeka, hali hii inatoa shinikizo kubwa kwa hali ya ajira nchini China."

    Bw. Yin hakudokeza idadi halisi ya wafanyakazi ambao watapoteza ajira kutokana na hatua za mageuzi, lakini amesisitiza kuwa serikali ya China itatenga yuan bilioni 100 kuwapanga wafanyakazi watakaopoteza ajira.

    "Kwa wale wafanyakazi watakaopoteza ajira, serikali ya China inahamasisha kampuni zenyewe zijitahidi kuwapanga, yaani kuvumbua nafasi mpya za ajira kutokana na vifaa na teknolojia zilizo nazo, ili kuwawezesha baadhi ya wafanyakazi hao waendelee kufanya kazi kwenye kampuni hizo. Aidha, China pia itatoa msaada kwa wafanyakazi watakaoondoka kabisa kwenye viwanda walivyofanya kazi, kama vile kuwapatia mafunzo ya kikazi, ili kuwasaidia waweze kupata ajira au kujiajiri haraka iwezekanavyo."

    Akizungumizia suala la ajira kwa wanafunzi wahitimu ambao idadi yao imeongezeka zaidi mwaka huu, Bw. Yin Weimin amesema China pia itachukua hatua mbalimbali kuwasaidia kupata ajira, zikiwemo kujitahidi kuvumbua nafasi mpya za ajira, kuwapatia mafunzo ya kikazi na kuwahamasisha wajiajiri.

    Bw. Yin amesema, hata hivyo wizara yake bado ina imani ya kudumisha utulivu wa hali ya ajira mwaka huu. Amesisitiza kuwa, uchumi wa China utaendelea kukua kwa uwiano, na kwenye mchakato huo, China pia itafanya mageuzi kwa muundo wa uchumi, ambapo sekta mpya zitavumbuliwa na nguvu mpya za msukumo zitajitokeza, hali ambayo pia itasaidia kwenye suala la ajira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako