Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania, Jarson Kalile wakati wa kongamano la wanaushirika Tanzania lililomalizika mwishoni mwa wiki.
Rais John Magufuli aliahidi kuondolea kwa wananchi kodi hasa kwa watu wenye kipato cha chini.
Jarson Kalile anasema jambo hilo limekuwa kikwazo kikubwa kwa wakulima hivyo harakati zao za kujikwamua kiuchumi kushindwa kuzaa matunda licha ya kutumia nguvu na rasilimali zao katika kilimo.
Alizitaja kodi hizo kuwa ni pamoja na ushuru wa halmashauri ya wilaya asilimia tano ya bei ya mkulima, ushuru wa utafiti asilimia 0.75 ya bei ya mnadani, mfuko wa maendeleo ya kahawa uliaonzishwa na wadau asilimia 0.5 ya bei ya mkulima, ada ya leseni ya kuuza kahawa nje zinazotozwa na Bodi ya Kahawa (TCB).
Kalile anasema hizo ni baadhi ya kodi na makato mbalimbali katika zao lakahawa na hali kama hiyo inajitokeza katika mazao mengine.
aidha walipendekeza kuondolewa kwa kodi za VAT kwa kuwa wakulima hulipa kodi hiyo asilimia 18 kwa mazao yao kama kusafirisha kahawa kutoka vyama vya msingi kwenda kiwanda cha kukoboa kahawa, magunia ya kuweka mazao yao na kukoboa kahawa yao kwenye kiwanda.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |