Msemaji wa ofisi inayoshughulikia kupunguza umaskini ya baraza la serikali ya China Su Guoxia amesema, mwaka jana idadi ya watu maskini vijijini nchini China ilipungua hadi milioni 55.75 kutoka milioni 70.17, na jukumu la kuwaondoa watu milioni 10 kutoka kwenye umaskini kwa mwaka lilikamilika vizuri.
Bibi Su Guoxia amefahamisha kuwa, mikoa na miji 22 ya katikati na ya magharibi mwa China imetoa ahadi kwa serikali kuu ya kukamilisha jukumu la kuondoa umaskini, na idara mbalimbali zimetoa sera na hatua nyingi zinazosaidia maendeleo ya sehemu na watu maskini.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |