• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Masuala ya uchumi yafuatiliwa zaidi na vyombo vya habari kwenye mikutano miwili ya China itakayofanyika

    (GMT+08:00) 2016-03-02 18:16:41

    Mkutano wa kwanza na waandishi wa habari wa Mkutano wa nne wa Baraza la 12 la mashauriano ya kisiasa la China umefanyika leo hapa Beijing. Msemaji wa mkutano huo Bw. Wang Guoqing amefahamisha kuhusu ajenda ya mkutano huo na kujibu maswali ya waandishi wa habari, ambayo mengi yanafuatilia maendeleo ya uchumi wa China.

    Tofauti na miaka iliyopita ambayo masuala ya kijamii yalifuatiliwa zaidi na vyombo vya habari kwenye mkutano wa Baraza la mashauriano ya kisiasa, kwenye mkutano huo, maswali matatu ya mwanzo yote yalikuwa yanafuatilia hali ya uchumi wa China, kama uchumi wa China unaweza kudumisha ongezeko la kasi au la? Msemaji wa mkutano huo Bw. Wang Guoqing amejibu kwa uhakika akisema.

    "Jibu ni ndiyo. Ingawa mwaka jana ukuaji wa uchumi wa China ulipungua, lakini kasi ya ongezeko la uchumi wa China bado ilikuwa inajitokeza sana ikilinganishwa na nchi nyingine duniani, na hali ya jumla ya utendaji wa uchumi wa China bado ni nzuri. Kwa upande wa ongezeko halisi la GDP au ufanisi wa ongezeko hilo, kasi ya asilimia 6.9 vyote vinaridhisha. Takwimu za utendaji wa uchumi za mwezi Januari mwaka huu pia zimetoa ishara nzuri, kwa hiyo kwa kukabiliana na hali yenye utatanishi ya uchumi wa dunia, bado tuna imani kubwa na uchumi wa China, Kwa sababu mwelekeo wa ukuaji wa uchumi bado haujabadilika, unyumbufu mkubwa na mustakbali wa uchumi wa China havijabadilika, msingi na mazingira imara ya kuunga mkono ukuaji endelevu wa uchumi wa China havijabadilika, na mwelekeo mzuri wa mageuzi ya muundo wa uchumi pia haujabadilika."

    Akizungumzia mageuzi ya mfumo wa huduma za afya yanayofuatiliwa na umma, Bw. Wang Guoqing amesema, mageuzi hayo ni mchakato mgumu wa muda mrefu, na Baraza la mashauriano ya kisiasa litafanya uchunguzi na kusikiliza maoni ya umma kwenye sehemu mbalimbali mwaka huu.

    "Mageuzi ya mfumo wa huduma za matibabu ni mchakato wa muda mrefu, mgumu na wenye utatanishi. Mageuzi hayo ni suala ngumu kwa nchi yoyote duniani, na ni gumu zaidi kwa nchi yetu kubwa yenye watu bilioni 1.3. Katika miaka ya hivi karibuni, Baraza la mashauriano ya kisiasa limefuatilia maendeleo ya mageuzi hayo, kila mwaka limefanya ukaguzi na uchunguzi, na kukutana kila baada ya wiki mbili. Mwaka huu, naibu wenyekiti watatu wa baraza letu wataongoza timu za ukaguzi kwenda sehemu mbalimbali nchini China, ili kujua hali halisi ya utendaji wa mfumo wa huduma za afya kwenye ngazi mbalimbali, na pia kukusanya maoni ya umma kuhusu mageuzi ya mfumo huo, ili kutoa ushauri na kuchukua hatua madhubuti kwa ajili ya kuendeleza vizuri mageuzi hayo."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako