• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa nne wa Baraza la 12 la mashauriano ya kisiasa la China wafunguliwa leo

    (GMT+08:00) 2016-03-03 18:43:38

    Mkutano wa nne wa Baraza la awamu ya 12 la mashauriano ya kisiasa la China umefunguliwa leo hapa Beijing. Akifungua mkutano huo kwa kutoa ripoti ya kazi za kamati ya kudumu ya baraza hilo, mwenyekiti wa baraza hilo Bw. Yu Zhengsheng amesema, mwaka huu baraza hilo litatoa kipaumbele kwenye kazi ya kutoa ushauri na mapendekezo kuhusu utekelezaji wa mpango wa 13 wa maendeleo ya miaka mitano.

    Mkutano wa nne wa Baraza la 12 la mashauriano ya kisiasa la China umefunguliwa rasmi leo saa 9 alasiri hapa Beijing. Kwenye mkutano huo wa siku 11, wajumbe zaidi ya 200 wa baraza hilo wanatoa ushauri na mapendekezo juu ya utekelezaji wa mpango wa 13 wa maendeleo ya mitano.

    Huu ni wa kwanza katika kipindi cha mwisho cha kukamilisha ujenzi wa jamii yenye maisha bora nchini China, na pia ni mwaka muhimu wa kuhimiza mageuzi ya muundo wa uchumi, ambapo mpango wa 13 wa maendeleo ya miaka mitano pia utaanza kutekelezwa rasmi. Kwenye ripoti yake, mwenyekiti wa baraza hilo Bw. Yu Zhengsheng ametoa maelekezo kwa kazi za baraza hilo kwa mwaka huu. Akisema,

    "Mwaka huu tutatoa kipaumbele kwenye kazi za kutoa ushauri na mapendekezo kuhusu utekelezaji wa mpango wa 13 wa maendeleo ya miaka mitano, kuweka mkazo katika kuongeza ufanisi wa mashauriano ya kisiasa, na kufuatilia majukumu muhimu ya kuhimiza mageuzi ya muundo wa uchumi. Pia tunatakiwa kutekeleza kwa makini mpango wa mashauriano kwa mwaka huu, kufanya ukaguzi na uchunguzi, na kujitahidi kupata matokeo yenye nguvu na uzito katika kazi za uchunguzi na mashauriano."

    Mbali na kufuatilia mchakato wa maendeleo, usimamizi wa kidemokrasia pia ni moja ya majukumu muhimu ya baraza hilo. Kwenye ripoti ya kazi za kamati ya kudumu ya baraza hilo, Bw. Yu Zhengsheng amesisitiza kuwa, katika mwaka huu mpya, baraza hilo linatakiwa kuongeza nguvu katika kutekeleza jukumu lake la usimamizi wa kidemokrasia, na kuinua zaidi ufanisi wa kazi hiyo.

    "Tunapaswa kufuatilia hatua muhimu za mageuzi zilizotolewa na kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China, na kufuatilia hali ya utekelezaji wa sera muhimu na utekelezaji wa vigezo vya udhibiti kwenye kipindi cha 13 cha maendeleo ya miaka mitano. Pia baraza letu linatakiwa kufanya ukaguzi na uchunguzi wenye lengo la usimamizi, ili kuimarisha ufanisi wa usimamizi wetu."

    Ripoti hiyo inasema, mwaka huu baraza hilo litawekea mkazo kazi za usimamizi wa kidemokrasia kuhusiana na mpangilio wa miji, ujenzi wa utaratibu wa kuhakikisha usalama wa chakula, ujenzi na usimamizi wa hifadhi za maumbile, pamoja na udhibiti wa uchafuzi wa hewa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako