Waziri mkuu wa China Li Keqiang amesema serikali itaendelea kuharakisha kilimo cha kisasa kwa kuongeza kiwango cha uzalishaji wa kilimo na kipato cha wakulima.
Hayo yalisemwa na waziri mkuu wa China Li Keqiang alipowasilisha ripoti ya kazi za serikali kwenye mkutano wa bunge la umma la China unaoendelea jijini Beijing.
Li amesema mwaka huu kilomita laki 2 za barabara mpya zitajengwa vijijini huku mtandao wa umeme na mabomba ya maji safi vitaimarishwa.
Li amesema ili kuelekeza mitaji kwenye sekta ya kilimo, mbali na bajeti kwa ajili ya kilimo, serikali itakamilisha mfumo wa mikopo ya dhamana na bima ya kilimo.
Waziri mkuu huyo amesisitiza kuwa mwaka huu lengo lililowekwa la kuwaondoa watu milioni 10 waishio vijijini kwenye umaskini lazima litatimizwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |