• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China asisitiza mageuzi na ufunguaji mlango

    (GMT+08:00) 2016-03-06 19:06:54

    Rais Xi Jinping wa China amesisitiza kuimarisha mageuzi na ufunguaji mlango.

    China itazalisha ma kuuza zaidi vifaa vya kisasa kwenye nchi zinazozojiunga na pendekezo la China la "Ukanda Mmoja na Njia Moja".

    Hayo yalisemwa na mkurugenzi wa kamati ya taifa ya maendeleo na mageuzi ya China, ambayo ni mamlaka inayosimamia upangaji wa uchumi wa China Bw. Xu Shaoshi kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika pembeni mwa mkutano wa bunge la umma la China unaoendelea jijini Beijing.

    Akizungumzia kwa undani ushirikiano wa kimataifa wa mwaka huu, Xu amesema uwezo wa uzalishaji wa viwanda na ujenzi wa reli utahamishwa zaidi.

    Xu ameongeza kuwa kutakuwa na uungaji mkono wa kifedha kwa ajili ya kuhimiza utekelezaji wa miradi husika.

    Mwaka jana, China ilifanya ushirikiano wa kiviwanda na nchi nyingi duniani, hasa katika sekta ya uzalishaji wa chuma na madini mengine, reli na uzalishaji wa umeme kwa nyuklia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako