• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapunguza lengo la ukuaji wa uchumi ili kuzidisha mageuzi

    (GMT+08:00) 2016-03-06 21:00:56
    Serikali ya China inalenga kasi ya ukuaji wa uchumi ya kati ya asilimia 6.5 hadi asilimia 7 kwa mwaka katika miaka mitano ijayo. Kasi hiyo itakuwa cha chini zaidi katika miongo tatu iliyopita. Hata hivyo, muundo wa uchumi wa China umeendelea kuboreshwa, ambapo sekta ya huduma imechukua zaidi ya asilimia 50 ya pato la jumla la taifa GDP kwa mara ya kwanza na uvumbuzi umekuwa injini mpya ya uchumi.

    Kwa kuweka malengo ya ukuaji ya uchumi kwa mwaka katika miaka mitano ijayo kuwa kati ya asilimia 6.5 na 7, serikali ya China inatoa nafasi ya kuwa na unyumbufu kwenye usimamizi wa uchumi, na pia kuacha nafasi ya mageuzi ya kimuundo ili kuwa na ukuaji wa muda mrefu.

    Kupitia hatua hiyo, serikali kuu imetoa ujumbe kwa viongozi wa serikali za mitaa kwamba haipaswi kuangalia kasi ya ukuaji wa uchumi peke yake. Ili kuwa na ukuaji wa uchumi ulio endelevu zaidi, mfumo bora wa kutathmini utendaji wa serikali za mitaa unapaswa kuanzishwa, ambao unatakiwa kushirikisha vigezo vya uhifadhi wa mazingira na vinginevyo.

    Hata hivyo hiyo haimaanishi kuwa malengo hayo hayana maana lakini kiwango cha chini zaidi cha asilimia 6.5 ni ukuaji unaohitajika katika kipindi cha miaka mitano ijayo ili kufikia lengo lililowekwa la kuwa na ukuaji maradufu kati ya mwaka 2010-2020.

    Na kiwango cha asilimia 7,ambacho ni chan juu kidogo ikilinganishwa na kiwango cha ukuaji cha asilimia 6.9 mwaka 2015, na una unaweza kuongeza imani kama utafanikiwa.

    Kufikia kiwango cha chini cha asilimia 6.5 ya ukuaji haitakuwa vigumu kwa China ambayo ina njia za kutosha za kuchochea ukuaji wa uchumi. Viwango vya riba bado ni vya juu ikilinganishwa na nchi nyingi zilizoendelea, na hivyo kuna uwezekano wa kuwa na kichocheo zaidi cha fedha kama inahitajika.

    Kiwango cha akiba ya wananchi bado ni kikubwa, hali ambayo inashiria nafasi kubwa katika siku za baadaye za matumizi na uwekezaji. Huku mapato ya wananchi yakipanda, idadi ya watu wenye mapato ya kati inaogezeka, na kundi hilo ndilo lenye uwezo mkubwa wa kununua.

    Changamoto zinazozikabili serikali za mitaa ni pamoja na nyumba zilizojengwa bila kununuliwa na marekebisho ya muundo wa viwanda ambayo yanaweza kuleta ukosefu wa ajira kama ule ulioshuhudiwa miaka ya 1990, wakati mageuzi ya viwanda vilivyomilikiwa serikali yaliacha wengi bila ajira.

    Kwa hiyo kuongeza nafasi za ajira kutapewa kipaumbele na serikali nyingi za mitaa wakati serikali kuu imeweka msisitizo mkubwa kwenye kazi hiyo.

    Jambo lilsiloepukika kwa sasa ni kwamba uchumi wa China umefikia hatua ya mageuzi ili kutimiza ukuaji endelevu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako