• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Oluoch apongezwa kwa wadhifa mpya

    (GMT+08:00) 2016-03-07 08:51:56
    Viongozi wengi wa michezo wamepongeza hatua ya serikali kumteua kamishna wa michezo Gordon Oluoch kuwa mkurugenzi mkuu wa Halmashauri ya Michezo (Sport Kenya)

    Oluoch amechukua wadhifa huo kutoka kwa Gabriel Komora, ambaye alikuwa ameshikilia nafasi hiyo kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita.

    Inadaiwa kwamba Komora atapewa wadhifa mwingine hivi karibuni katika idara ya michezo nchini.

    Kutokana na uteuzi huo, naibu kamishna wa michezo, Maina Kamau atachukua rasmi nafasi ya Oluoch.

    Mwenyekiti wa Chama cha Olimpiki Nchini (NOCK) Kipchoge Keino, Mwekahazina wa Baraza la Michezo Nchini (KNSC) Charles Nyaberi, na katibu mkuu wa chama cha Nock, Francis Paul wamepongeza uteuzi wa Oluoch na kusema ametosha kuhudumu katika wadhfa huo mpya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako