Wakati mkutano wa bunge la umma la China unaendelea hapa Beijing na serikali ya China inaendelea kuhimiza mageuzi ya muundo wa uchumi ili kuendana na hali mpya ya kawaida ya maendeleo ya uchumi, vyombo vya habari vya nchi mbalimbali duniani, vimekuwa vikieleza matumaini kwa uchumi wa China..
Gazeti la The New York Times la Marekani limesema, mwaka huu serikali ya China inarekebisha lengo lake la ongezeko la uchumi kuwa eneo fulani kutoka takwimu halisi, hii ni hatua inayopigwa katika mwelekeo sahihi.
Gazeti la Financial Times na shirika la habari la Reuters la Uingereza yamesema, mwaka huu ripoti kuhusu kazi za serikali ya China imetoa bajeti yenye nakisi inayolingana na pato la taifa, ambayo imeongezeka hadi asilimia 3 kutoka asilimia 2.3 ya mwaka jana. Hii inamaanisha kuwa ingawa serikali inataka kupunguza athari ya kudidimia kwa uchumi bila kutumia hatua za kuchochea mambo ya kifedha.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |