• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China asema msukumo mpya utahimiza ongezeko la uchumi

    (GMT+08:00) 2016-03-07 10:54:48

    Waziri mkuu wa China Bw Li Keqiang ametoa mwito wa kuwepo kwa msukumo mpya ili kuhimiza ongezeko la uchumi, na kusema China ina uwezo wa kutimiza malengo ya ongezeko la uchumi na maendeleo ya kijamii.

    Akiongea kwenye kikao cha pembeni cha mkutano wa bunge la umma, waziri mkuu Li amewaambia wabunge kuwa mafanikio ya kiuchumi na kijamii ya mwaka jana, yameimarisha imani kuwa changamoto yoyote inaweza kutatuliwa.

    Bw Li amesema China inataka kulinda ongezeko la wastani na juu la uchumi na kuelekea kwenye kiwango cha maendeleo ya wastani na juu. Bw Li amekumbusha kuwa China itaendelea na mageuzi ya kimuundo, hasa kwenye eneo la utoaji wa bidhaa na kutekeleza mkakati unaoongozwa na uvumbuzi.

    Waziri mkuu pia amesema elimu, huduma za afya, nyumba, uhakikisho wa jamii na usalama wa chakula, pia ni mambo yanayopewa kipaumbele kwenye utendaji wa serikali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako