• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China asema kasi mpya itaboresha ukuaji wa uchumi

    (GMT+08:00) 2016-03-07 19:24:11
    Waziri mkuu wa China Li Keqiang amesema ana imani na utendaji wa uchumi wa China katika siku za mbele.

    Li amesema hayo alipokutana na wabunge wanaotoka mkoa wa Shandong wanaohudhuria mkutano wa bunge la Umma la China. Li amesema:

    "Katika kipindi hiki cha mpito, mahitaji makubwa tena mapya yanaibuka nchini China. Mageuzi ya sasa ndiyo yanalenga kuweka upatikanaji zaidi ya mahitaji hayo kupitia uvumbuzi. Makampuni madogo yanayotoa huduma za nyumbani, na huduma za matunzo ya wazee yatakuwa na faida kubwa na kubuni nafasi zaidi za ajira kuliko makampuni makubwa, kama tutafanikiwa kuondoa vizuizi vya maendeleo kwa makampuni hayo madogo."

    Li pia amesema hatua zinachukuliwa ili kujaribu kuunganisha kampuni, vyuo vikuu, na taasisi za utafiti ili kusaidia kukuza uchumi.

    Mkutano wa bunge la umma la China umeingia siku ya tatu, ambapo viongozi wa taifa wakiwemo rais Xi Jinping na waziri mkuu Li Keqiang wameshiriki kwenye vikao vya wabunge kutoka mikoa mbalimbali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako