Lengo hilo limetajwa kwenye muswada wa mpango wa 13 wa maendeleo ya miaka mitano ya uchumi na jamii ya China.
Akizungumzia lengo hilo, waziri wa kilimo Han Changfu amesema, wizara yake itachukua hatua husika za kusaidia kulitimiza lengo hilo, ambazo ni pamoja na sera nafuu za kifedha, kuongeza ufanisi wa uzalishaji wa familia, kuunganisha nguvu za wakulima, na kuhimiza usawa wa huduma kati ya mijini na vijijini.
Akizungumzia maendeleo ya kilimo cha kisasa, Han amesema maendeleo hayo yanasukumwa kwa asilimia kubwa na uvumbuzi wa teknolojia, na mwaka jana teknolojia ilichangia asilmia 56 ya ukuaji wa kilimo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |