• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa China wahimiza kuendeleza mageuzi na kuimarisha utawala wa Chama cha Kikomunisti

    (GMT+08:00) 2016-03-08 10:01:50

    Mkutano wa bunge la umma la China unaendelea hapa Beijing, na viongozi wakuu wanaoshiriki kwenye vikao mbalimbali vya mkutano huo, wamekuwa wakiongelea mambo mbalimbali yanayopewa kipaumbele na serikali kuu.

    Rais Xi Jinping wa China amewataka wajumbe kutoka mkoa wa Kaskazini Mashariki ambao ngome ya zamani ya viwanda, wazingatie kubadilisha mtindo wa uzalishaji, bei za chakula, kupambana na umaskini na kuufanyia mageuzi muundo wa uchumi.

    Rais Xi Jinping pia amesema maofisa wa serikali za mitaa na wa chama wanatakiwa kufuata sheria wakati ya kutekeleza sera za mageuzi, na kutaka maofisa wenye uwezo na waaminifu wazawadiwe kwa kupandishwa vyeo

    Waziri Mkuu wa China Bw Li Keqiang aliyeongea na wajumbe kutoka mkoa wa Fujian, amewaagiza kuimarisha shughuli za kilimo na uvuvi, na kuweka msingi kwa maendeleo ya eneo la pwani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako