Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema mkutano wa kilele wa kundi la G20 utakuwa na umuhimu wa kidiplomasia kwa China katika mwaka huu, na ni mkusanyiko kuhusu uchumi utakaofuatiliwa zaidi duniani, na mkutano huo utaweka kipaumbele kwa kazi za kutafuta nguvu mpya zinazotokana na uvumbuzi, kuingiza uhai mpya kupitia mageuzi, na kujenga mustakbali mzuri kwa njia ya maendeleo.
Bw. Wang amesema hayo alipohojiwa kuhusu jinsi China itakavyoonesha umuhimu wa uongozi katika kuandaa mkutano wa G20 utakaofanyika mjini Hangzhou, mashariki mwa China. Amesema ongezeko linalohimizwa na uvumbuzi litakuwa ajenda muhimu kwenye mkutano huo na China inatarajia kutumia fursa zinazotokana na mapinduzi mapya ya kiviwanda na uchumi wa kidigitali ili kupanga mpango mpya kwa ajili ya ukuaji wa uchumi wa dunia. Ameongeza kuwa China inapenda kuhimiza makundi makuu ya kiuchumi duniani kufikia makubaliano kuhusu umuhimu wa mageuzi ya kimuundo na pia nchi wanachama wa kundi la G20 watahamasishwa kutunga mipango ya utekelezaji wa ajenda ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa kuelekea mwaka 2030 ili kuleta maendeleo ya pamoja duniani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |