• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Diplomasia ya nchi kubwa ya China imeanza kuonekana chini ya uongozi wa rais Xi Jinping

    (GMT+08:00) 2016-03-08 11:21:28

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema diplomasia ya nchi kubwa yenye umaalumu wa Kichina imeanza kuonekana tangu rais Xi Jinping aingie madarakani.

    Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari pembeni mwa mkutano wa mwaka wa bunge la umma la China, Bw. Wang amesema juhudi za kidiplomasia za China zinasaidia kutimiza ndoto za China zinazolenga ustawi wa taifa na kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja kwa binadamu wote kupitia chaguo la kimkakati la maendeleo yenye amani. Wang pia amesema kanuni za kimsingi ni kuwa na ushirikiano unaolenga kunufaika kwa pamoja na kujenga aina mpya ya mahusiano ya kimataifa kwenye msingi huo, na njia kuu ni kujenga aina mbalimbali za uhusiano wa kiwenzi na kuchagua wenzi bila kufungamana na kufanya mazungumzo badala ya mapambano.

    Ameongeza kuwa thamani inayosisitizwa na China ni kushikilia njia yenye uwiano kwa urafiki na maslahi, kutetea haki kwenye masuala ya kimataifa na kuweka kipaumbele urafiki kabla ya maslahi katika mahusiano kati ya mataifa mawili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako