• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Opera ya kijadi ya mkoa wa Guangdong, ulioko pwani ya kusini ya China

    (GMT+08:00) 2016-03-08 15:22:42

    Kwenye sehemu ya kusini ya China kuna mji mmoja wenye historia ya zaidi ya miaka 2200, unaoitwa Guangzhou. Mji huo uliwahi kuwa mji mkuu wa enzi tatu katika historia, uliwahi kuwa kituo cha kwanza kwa meli za kigeni zilizoingia China, sasa umekuwa bandari kubwa kabisa ya biashara na nje, yenye historia ndefu zaidi nchini China. kwa hiyo, mji wa Guangzhou unasifiwa kuwa ni "mji wa biashara wa milenia". Kutokana na hali yake maalumu ya kijiografia na kihistoria, mji huo pia ni sehemu inayofungua mlango zaidi kwa nje na kuchanganya utamaduni wa China na wa kigeni.

    Uliyosikia ni lahaja ya kienyeji inayotumiwa sambamba na kichina sanifu mandarini mjini humo, inaitwa Cantonese. Lahaja hiyo inayotumiwa kote mkoani Guangdong, lakini ile inayotumiwa mjini Guangzhou ni sanifu zaidi. Lahaja hiyo inatumia maneno mengi ya kichina ya kale, ina sauti tano zaidi kuliko mandarin, na zaidi ya nusu ya maneno yake ni ya kienyeji, kwa hiyo matamshi ya lahaja hiyo yanapendeza lakini ni magumu kujifunza. Hivi sasa, zaidi ya watu milioni 100 duniani wanatumia lahaja hiyo, hasa wakazi wa peninsula ya mto wa Zhujiang, Hongkong, Macau na wachina wanaoishi ng'ambo. Muziki na opera ya kiguangdong yenye historia ya zaidi ya karne moja zote zimeathiriwa kwa kina na lahaja hiyo.

    Opera ya kiguangdong iliyoanzishwa huko Foshan, ni opera ya kienyeji yenye mashabiki wengi zaidi mkoani Guangdong, mpaka sasa imekuwa na historia ya zaidi ya miaka mia tatu. Opera hiyo inayoimbwa kwa lahaja ya kikanton, ni opera ya kwanza ya China iliyooneshwa katika nchi za nje. Mwaka 1852, bendi ya opera ya Hongfutang kutoka Guangdong ilionyesha opera hiyo mjini San francisco, Marekani, ikilinganishwa na opera ya kibeijing iliyooneshwa mara kwa kwanza nje ya China mwaka 1930. Miongoni mwa opera za jadi za kichina za aina zaidi ya mia tatu, opera ya kiguangdong ilitambuliwa rasmi tarehe 30 Septemba mwaka 2009 na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa kuwa ni urithi wa kiutamaduni usioonekana duniani, ambayo ni opera ya pili ya China kutambuliwa na shirika hilo baada ya opera ya Kunqu.

    Bi. Chen Shaomei amefanya kazi zinazohusiana na opera hiyo kwa zaidi ya miaka 50, na aliwahi kuwa mchezaji, mtungaji na mwongozaji wa opera hiyo. Bi. Chen anaona kuwa Guangzhou ni mji wa bandari wa milenia, umaalumu wa mji huo wenye kufungua mlango na uvumilivu pia unaonekana kwenye opera hiyo.

    "Opera ya kiguangdong ina sauti nyingi kabisa miongoni mwa opera zaidi ya mia tatu za China, baadhi ya sauti zinatoka opera za mikoa mingine, nyimbo za Hong Kong na hata nyimbo za mandarin. Tunaweza kuingiza sauti yoyote kama ikipendwa na watazamaji. Kwa sababu Guangzhou ni mji wa bandari, ufunguaji na uvumilivu ni umaalumu mkubwa wa oprea ya Kiguangdong."

    Mbali na hayo, opera ya kiguangdong pia inatumia nyimbo za kigeni na ala za magharibi kama vile violin.

    Opera ya kiguangdong inapendwa na watu wengi, hasa wazee, kwenye sehemu inayotumia lahaja ya kiguangdong. Kwa kawaida, marafiki wanaunda bendi yao wenyewe na kucheza opera hiyo katika bustani, au uwanja.

    Mwandishi wetu alitembelea bendi moja yenye historia ya miaka 31, ambayo sasa ina wachezaji 20-30, kila wiki wanakutana mara tatu na wanaimba na kucheza opera hiyo. Mkuu wa bendi hiyo Bw. Jian Guoxin anasema, bendi hiyo ni sehemu isiyokosekana ya maisha yake, wakati ilipoanzishwa, yeye alikuwa bado ni kijana, sasa ameshastaafu na kila siku anaendelea kutafuta siri ya opera hiyo.

    "Muziki wa pop unakaa vilevile kama ilivyotungwa. Lakini kila wimbo wa opera ya kiguangdong utaweza kuucheza kwa mtindo tofauti katika kila maonesho, kwa sababu kuna mitindo mingi ya kuigwa, waimbaji nyota pia wana mitindo yao tofauti. Napenda sana mabadiliko hayo."

    Sanaa ya opera ya kiguangdong si kama tu imevutia mashabiki kuunda bendi za kienyeji, bali pia imevumbua muziki wa mtindo wa kiguangdong. Ukitembelea mjini Guangzhou, mahali popote bila kujali ni mtaani, uwanjani, au hotelini, muziki wa kiguangdong utasikika, na kukuburudisha kwa mtindo wake maalumu wa kienyeji.

    Katika kipindi kirefu cha kihistoria, muziki wa kiguangdong ulichukuliwa nchini hata duniani kuwa ni "muziki wa kitaifa wa China". Mwaka 1954, muziki wa Guangdong ulisifiwa na mwanamuziki mmoja wa Urusi ya zamani kuwa ni "muziki wazi", yaani ukifumba macho, unaweza kupata undani wake akilini mwako mara maja.

    Msemo wa kale unasema, ardhi tofauti inalea watu tofauti, na lahaja tofauti pia inabuni utamaudni tofauti. Bw. Tang Kaixuan ni mrithi wa muziki wa kiguangdong ambao ni urithi wa kiutamaduni usioonekana wa China. Akitoa mfano, alisema, muziki wa Kiguangdong ni kama kitoweo cha kiguangdong, inakubidi uonje polepole, ndipo utagundua tofauti za ladha yake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako