• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Spika wa Bunge la Umma la China asisitiza kuhimiza maendeleo na utawala bora kwa kutumia sheria

    (GMT+08:00) 2016-03-09 18:31:43

    Spika wa Bunge la Umma la China Zhang Dejiang asisitiza umuhimu wa kuhimiza maendeleo na utawala bora kwa kutumia sheria.

    Zhang alisema hayo alipotoa ripoti ya kazi ya kamati ya kudumu ya bunge kwa wabunge wote kwenye mkutano wa mwaka wa bunge hilo unaoendelea jijini Beijing.

    Ripoti hiyo imeonesha kuwa kipaumbele cha kazi ya utungaji wa sheria kwa mwaka huu, ni kuharakisha kukamilisha mfumo wa sheria ili kuhimiza utekelezaji wa mtazamo mpya wa maendeleo.

    Utungaji au marekebisho ya sheria nyingi zimewekwa katika mpango wa kazi ya mwaka huu. Sheria hizo ni pamoja na Kanuni kuu za sheria ya kiraia, sheria ya kodi ya hifadhi ya mazingira, sheria ya tathmini ya mali, sheria ya hisa na sheria ya kuhimiza kampuni ndogo na za wastani.

    (Sauti 1)

    "Tangu mwaka jana, kamati ya kudumu ya bunge imetunga sheria 5, kurekebisha sheria 37, kukagua utekelezaji wa sheria 6 na kupitisha mikataba na makubaliano na nchi za nje na kujiunga na mikataba 11 ya kimataifa."

    Mwaka jana, utungaji au marekebisho ya sheria kadhaa yalikuwa yakifuatiliwa sana nchini China. Utungaji wa sheria ya usalama na sheria ya kupambana na ugaidi imeziba pengo katika utungaji wa sheria wa sekta ya usalama wa taifa la China. Marekebisho ya sheria ya usalama wa chakula, sheria ya kuzuia na kudhibiti uchafuzi wa hewa na sheria ya idadi ya watu na mpango wa uzazi ziliitikia ufuatiliaji wa raia, na kuwa na athari kubwa kwa maendeleo ya uchumi na jamii ya China.

    Mwaka huu ni kipindi muhimu cha China kujenga jamii yenye neema kwa pande zote, na pia ni mwanzo utekelezaji wa mpango wa 13 wa maendeleo wa miaka mitano ya uchumi na jamii. Bw. Zhang amesema, mwaka huu kamati hiyo itaendelea kuimarisha utungaji wa sheria, na kuharakisha kuunda mfumo wa kamili wa sheria.

    (Sauti 2)

    "Kamati ya kudumu itatekeleza kwa makini sheria iliyorekebishwa kuhusu utungaji wa sheria na mpango wa utungaji wa sheria, kurekebisha, au hata kufuta sheria zisizofaa na kutoa ufafanuzi kuhusu marekebisho, ili kutekeleza ipasavyo mtizamo mpya kuhusu maendeleo. Pia inatakiwa kukamilisha sheria za kiuchumi, kiutamaduni na kijamii, kujitahidi kufanya kila utungaji wa sheria ulingane na moyo wa katiba na ufuatiliaji wa wananchi. "

    Ripoti hiyo inaonesha kuwa mwaka huu bunge la China litatunga sheria mbalimbali zikiwemo sheria ya nafaka, sheria ya huduma ya utamaduni ya umma, na sheria ya uhimizaji wa sekta ya filamu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako