• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mjasiriamali kijana Zhang Chao

    (GMT+08:00) 2016-03-10 08:16:25

    Bw. Zhang Chao ni kijana aliyezaliwa mwaka 1985 hapa Beijing, sasa yeye ni mmoja wa waanzilishi wa tovuti ya Kanjia, ambayo inashguhulikia mauzo ya nyumba. Baada ya kuhitimu kutoka chuo kikuu, aliwahi kuwa mtengeneza progamu za kompyuta. Mwaka 2011 alianza kujishughulisha na biashara ya nyumba. Baada ya miaka mitatu, pamoja na uzoefu wake mwenyewe wa kupanga na kununua nyumba, Bw. Zhang Chao alitambua dosari mbili kubwa kwenye biashara ya nyumba, yaani kutokuwa na taarifa sawa kati ya wauzaji na wanunuzi wa nyumba na huduma mbaya kwa wateja. Kwa hiyo mwaka 2014, Bw. Zhang Chao na marafiki zake walifikiria kuanzisha kampuni ya biashara za nyumba. Anatarajia kuwa siku moja kupitia nguvu yake ataweza kufanya shughuli za biashara za nyumba zibadilike na kuwanufaisha zaidi wateja.

    Mwaka 2014 bei ya nyumba nchini China ilikuwa inashuka kwa kiwango kikubwa, na soko la nyumba lilibadilika kuwa soko la wateja kutoka soko la wauzaji, hali ambayo ilizusha mahitaji makubwa kwa uwazi wa taarifa za biashara ya nyumba na huduma bora kwa wateja. Tovuti ya Kanjia ndio ilianzishwa kwenye mazingira hayo. Bw. Zhang Chao anasema kuanzishwa kwa tovuti ya Kanjia kulikuwa na lengo la kutoa machaguo mengi zaidi kwa wateja, si kama tu kuwapatia wateja habari zilizo wazi na za kweli, bali pia kutoa huduma bora zaidi. Bw. Zhang anasema,

    "Kama ukitaka niweke alama mbili kwa tovuti ya Kanjia, basi moja ni habari, ni za kweli kabisa na tena ziko wazi, nyingine ni huduma, katika sekta hiyo ya biashara za nyumba, tunafanya juhudi kutoa huduma bora zaidi."

    Kwa Bw. Zhang Chao na tovuti yake ya Kanjia, mwaka 2014 ulikuwa mwaka usio wa kawaida. Katika mwaka huo, kampuni yake ilifanikiwa kubadilika kutoka kampuni ya kawaida ya wakala wa nyumba, na idadi ya wafanyakazi wake pia iliongezeka hadi kuwa mamia kutoka chini ya mia moja. Hasa mwishoni mwa mwaka 2014 mafanikio ya kukusanya fedha yalifanya kampuni hiyo iendelezwe kwa kasi kubwa. Kadiri idadi ya wafanyakazi ilivyokuwa inaongezeka kwa kasi, ndivyo upangaji wa kundi la uendelezaji wa tovuti ya Kanjia uliboreshwa. Bw. Zhang anasema,

    "Hivi sasa tuna makundi matatu. Moja ni kundi la OFFLINE, la pili ni kundi la ONLINE nililoko mimi, ambalo linawasiliana zaidi na idara za kushughulikia mtandao wa internet, lingine ni idara za kutoa uungaji mkono, zikiwemo idara inayoshughulikia raslimali za nguvukazi, idara ya fedha na idara ya usimamizi wa jumla."

    Kwa kawaida, mfanyabiashara wa nyumba anahitaji kushughulikia kazi mbalimbali mwenyewe ikiwemo kutafuta na kuwahudumia wateja, na kazi hizo nyingi zinaathiri sana ubora wa huduma. Kwa hiyo tovuti ya Kanjia ilifanya upangaji mzuri kwa kazi za idara mbalimbali, pia inaunda idara maalum ya usimamizi wa huduma ili kufanya usimamizi na tathmini ya ubora wa huduma zinazotolewa na wafanyakazi wa kundi la OFFLINE kwa wateja, na mshahara wa wafanyakazi utatolewa kwa mujibu wa idadi ya wateja wanaoridhika na huduma zao na alama wanazotoa wateja. Hii pia ni tofauti kati ya kampuni ya kawaida ya wakala wa nyumba na kampuni ya biashara za nyumba kwa mbinu ya O2O yaani kwa kiingereza "Online to Offline". Bw. Zhang Chao anasema,

    "Hatutoi asilimia ya faida kwa wafanyakazi wetu kwa mujibu wa idadi ya nyumba wanazouza, bali tunaangalia kiwango cha kuridhika kwa wateja kuhusu huduma wanazotoa wafanyakazi wetu. Kama mfanyakazi anauza nyumba 100 lakini wateja hawaridhiki huduma yake, hatapewa asilimia nyingi ya faida kuliko mwingine anayeuza nyumba kadhaa tu lakini wateja wanampa alama 100 kwa huduma yake. Hatua hii inaweza kuwahimiza wafanyakazi wetu wawahudumie vizuri zaidi wateja, na kutoa kipaumbele kwa huduma zao."

    Bw. Zhang Chao anaona kuwa, mfanyakazi bora si kama tu ana ujuzi mwingi na uzoefu mkubwa, bali pia anahitaji kuwa na uwezo mkubwa wa kuwa na moyo wa kujifunza. Bw. Zhang mwenyewe ni mfano wa mtu mwenye moyo wa kujifunza, kila wiki anatumia asilimia 40 ya muda wa kazi kujifunza. Bw. Zhang anasema,

    "Naona wajasiriamli, hawana uzoefu wa kuigwa, kwa hiyo inanihitaji kujifunza mimi mwenyewe. Kwa kawaida, najifunza kwanza, halafu ninaandaa Power Point na kuwafundisha wengine. Kila wiki tuna muda maalum, ambapo mmoja anawafundisha wengine. Naona kama kampuni ikitaka kufanya kazi vizuri, inahitaji wafanyakazi wake kujifunza taaluma, na sisi tukiwa wasimamizi tunapaswa kujifunza zaidi."

    Kuanzia mwaka 2014 kampuni hiyo ilipoanzishwa hadi sasa, ingawa huduma inazotoa zinabadilika badilika, lakini madhumuni ya mwanzo ya kundi hilo hayabadiliki, yaani "kuwanufaisha zaidi wateja". Hii ni njia mpya ambayo haina uzoefu wa kuigwa, hivyo kampuni inahitaji kufanya majaribio na kujiboresha siku zote, Bw. Zhang Chao anaona kuwa hili ni jambo ambalo kampuni yake inastahili kufanya juhudi. Bw. Zhang anasema,

    "Tuko upande wa wateja wetu na tunawahudumia, huu ni mwelekeo wa maendeleo ya jamii. Kama bila sisi, basi katika siku za usoni pia kutakuwa na makampuni mengine kufanya kazi hiyo, kwani hivi sasa mchakato wa kuendeleza miji umeendelezwa sana, na polepole soko linaloamuliwa na wauzaji limebadilika kuwa soko linaloamuliwa na wateja, na tukifanya kazi hiyo miaka mitatu iliyopita au miaka mitatu ijayo haifai, sasa ni muda mwafaka."

    Ingawa tovuti ya Kanjia bado iko katika kipindi cha mwanzo cha maendeleo yake, moyoni mwa Bw. Zhang Chao kuna mpango mkubwa wa kuendeleza tovuti hiyo. Katika mpango huo, tovuti ya Kanjia itatoa mchango katika kusimamia masoko ya nyumba ya miji mingine mingi. Bw. Zhang anasema,

    "Kama tukitaka kuchuma pesa tu, basi itakuwa rahisi zaidi, lakini kwa nini tunataka kueneza katika miji mingine mingi? Kwa sababu hivi sasa Beijing umekuwa moja ya miji yenye utaratibu mzuri zaidi nchini China, lakini kwa miji midogo na yenye ukubwa wa kati ambayo ndiyo medani yetu muhimu, masoko ya nyumba ya miji hiyo hayakusimamiwa vizuri, watu wa huko hawana uhakikisho wowote, na tunalotaka kufanya ni kuwafanya wateja wasihangaike. Kama unataka ubaki katika miji mikubwa kwa starehe tu, basi hakuna maana yoyote."

    Ingawa wakati kampuni inapoendelezwa hukumbwa na matatizo mbalimbali, ingawa aliwahi kuwa na wazo la kuacha juhudi zake, lakini, akifirikia ndoto yake na mustakbali wa siku za baadaye, Bw. Zhang Chao na kundi lake waliamua kuendelea na shughuli zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako