Mjumbe wa baraza la mashauriano ya kisiasa la China Bw. Xie Zhenhua amesema, kufanya juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, ni mahitaji ya China katika kujiendeleza bila uchafuzi, na pia kunaonesha majukumu ya China kwenye ushiriki wa usimamizi wa dunia, na wajibu wake wa kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja kwa binadamu wote.
Bw. Xie Zhenhua amependekeza kuwa China inapaswa kuimarisha sera na hatua za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa katika miaka mitano ijayo, ili kutimiza lengo la kupunguza utoaji wa hewa Carbon dioxide kwa asilimia 45 hadi mwaka 2020 kuliko mwaka 2005. Wakati huo huo China inatakiwa kuhimiza utungaji wa sheria kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, kuiga uzoefu wa nchi nyingine, ili kuhakikisha msingi wa sheria kwa shughuli mbalimbali za kujiendeleza bila uchafuzi.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |