Waziri wa elimu wa China Bw. Yuan Guiren amesema maendeleo ya elimu nchini China yanafanana au yamezidi kiwango cha nchi zenye mapato ya wastani hadi juu duniani.
Amesema kwa mujibu wa tathmini iliyofanywa na taasisi ya upande wa tatu, asilimia 75 ya watoto wa China wanajiunga na chekechea, kiasi hiki ni sawa na wastani wa nchi zenye mapato ya wastani hadi juu. Asilimia 99.9 ya watoto wanajiunga na shule ya msingi, na asilimia 100 wanaojiunga na shule za sekondari .
Waziri huyu amesema kiwango cha watoto wanaopata elimu ya lazima ya miaka tisa nchini China kimezidi kile cha wastani wa nchi zenye mapato ya wastani hadi juu. Asilimia 87 ya vijana wa China wanasoma katika shule ya sekondari ya juu, na asilimia 40 wanapata elimu ya juu vyuoni.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |