Mjumbe wa Baraza la 12 la Mashauriano ya kisiasa la China Bw. Bo Shaoye amesema, utafiti uliofanyika nchi nzima unaonyesha kuwa, idadi kubwa ya walemavu nchini China wanaishi chini ya mstari wa umaskini katika maeneo ya vijijini. Kutokana na uhaba wa nafasi za ajira na huduma za afya, kwa wastani, walemavu hao wanapata nusu ya wastani wa kipato cha wananch wengine.
Bo amesema, serikali inatakiwa kufuatilia suala la nyumba kwa walemavu, pamoja na bima ya jamii na mafunzo ya ufundi, ili kuwawezesha kupata nafasi za ajira.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |