• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yavitoza viwanda vilivyochafua mazingira faini zaidi ya dola milioni 650 za kimarekani

    (GMT+08:00) 2016-03-11 21:10:17
    Waziri wa uhifadhi wa mazingira Chen Jining amesema mwaka jana viwanda vinavyochafua mazingira nchini China vilitozwa faini dola milioni 650 za kimarekani, ikiwa na ongezeko la theluthi moja ikilinganishwa na mwaka 2014.

    Chen amesema kati ya viwanda vilivyofanyiwa uchunguzi, vingine vilotozwa faini huku vingine vikisimamishwa uzalishaji au hata kufungwa.

    Amedokeza kuwa bunge la China linaandaa mswada wa sheria ya kodi ya uhifadhi wa mazingira, ambayo inalenga kutoza kodi zaidi wachafuzi wakubwa.

    Waziri huyo amesisitiza kuwa tofauti na inavyodhaniwa, uhifadhi wa mazingira na maendeleo hazipingani, zinaweza kwenda sambamba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako